MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wenye Ulemavu Wa Ngozi Wakumbukwa Kupitia FDH, Wapewa Msaada Wa Milioni 20
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wenye Ulemavu Wa Ngozi Wakumbukwa Kupitia FDH, Wapewa Msaada Wa Milioni 20
Habari

Wenye Ulemavu Wa Ngozi Wakumbukwa Kupitia FDH, Wapewa Msaada Wa Milioni 20

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: WATU wenye ulemavu wa ngozi Mkoani Dodoma  wamepatiwa msaada wa vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia kupambana na hali yao ya ulemavu.
Benki ya NMB imetoa vitu mbalimbali yakiwemo  mafuta maalum kwa ajili ya kujikinga na mionzi ya jua inayosababisha saratani ya ngozi kwa watu hao.
Meneja wa NMB Kanda ya kati Janeth Shangwe, akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya watu wenye ulemavu ya Foundation For Disabilities Hope (FDH), Maiko Salali amesema  tukio hilo ni sehemu ya kutekeleza takwa na taasisi kuresha kwa jamii kile wanachokipata.
“Sisi kama NMB kutoa msaada kwa jamii imekuwa ni jambo letu na tumekuwa tukithamini watu wa aina mbalimbali,
“Tulipo pata maombi yenu kuwa mnahitaji vifaa kwa ajili ya kujingia na mionzi ya jua mara moja tuliona kuna umuhimu mkubwa kushirikiana na tutumie sehemu ya faida ambayo tunaipata kwa ajili ya kuleta msaada huu.
“Tunaamini kwa namna moja ama nyingine nyinyi kama Foundationa For Disabilities Hope hapa Dodoma mtaufikisha msaada huu kwa wengi ambao wanauhitaji na vitu hivi,” amesema.
Ametaja vifaa walivyotoa ni mafuta ya kujikinga na mionzi ya jua 200, kofia za jua 200 pamoja na miwani ya jua 200 vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 20.
Kwa upande wake  Mkurugenzi Mtendaji wa FDH, Maiko Salali ameishukuru NMB, na kueleza jinsi benki hiyo inavyogusa makundi ya wenye ulemavu.
“Kupitia msaada huu mmerejesha matumaini kwa watu wenye ulemavu msaada huu kwetu sisi watu wenye ualibino mmetusaidia kuongeza kiwango cha kuishi sisi watu wenye ualibino tunakabiliwa na changamoto ya saratani  ya ngozi, adui yetu namba moja ni jua,”amesema.
Amesema, mionzi ya jua inapowapiga kwenye ngozi wanatokwa na vidonda ambavyo badae vinakwenda kusababisha saratani ya ngozi.
“Hivyo hivi vifaa vya kujikinga na mionzi ya jua vinakwenda kuimarisha maisha yetu na kuweza kushiriki katika kulijenga taifa letu,” amesema.

You Might Also Like

Waziri Mkuu Kumwakilisha Dkt Samia Ivory Coast

Jackline Mzindakaya: Uteuzi wa Mwigulu Ni Chaguo Sahihi kwa Taifa

HATUNA HURUMA NA WADANGANYIFU KWENYE MITIHANI – WAZIRI MKENDA

Mbunge Kuchauka azindua kambi kuhamasisha Uchaguzi Serikali za  Mitaa

Madaktari Bingwa, Wauguzi Wabobevu Wa Mama Samia Watoa Mafunzo Ya Huduma Kwa Mama Na Mtoto, Hospitali Ya Wilaya Ya Singida

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article JOWUTA,IFJ na THRDC kutoa mafunzo ya kuripoti uchaguzi mkuu.
Next Article Waziri Mkuu Majaliwa Ahimiza Watanzania Kufanya Mazoezi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?