Na Mwandishi Wetu
KIGOMA: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amevutiwa na utafiti uliofanywa na mhitimu wa Shahada ya Uzamivu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, (OUT), Marehemu Billy Mwakatage, uliohusu majanga ya moto.
Kutokana na kuvutiwa na utafiti huyo, Majaliwa ameiagiza Idara ya Menejimenti ya Maafa na Jeshi la Zimamoto kutumia mapendekezo yaliyomo kwenye utafiti huo katika kukabiliana na majanga nchini.
Waziri Mkuu, ametoa wito huo Disemba tano, 2024 katika mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambapo alimwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango yaliyofanyika katika viwanja vya Kawawa Manispaa ya Kigoma-Ujiji.

Shahada hiyo imepokelewa na Mjane wa Marehemu Ningile Kapange baada ya mumewe Mwakatage kufariki kabla ya kutunukiwa shahada yake.Waziri mkuu Majaliwa amesema utafiti wake una mahusiano makubwa na shughuli inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa katika kudhibiti maafa na majanga mbalimbali.
“Kwa kuwa ameshahitimu na leo anapata shahada na amefanya utafiti wa kina kwenye eneo la maafa na hasa majanga ya moto ambayo wakati wote serikali tumekuwa tukipambana nayo, “Msomi wetu Marehemu Billy Mwakatage pamoja na utafiti ametoa mapendekezo mbalimbali, utafiti huu uchukuliwe na ufanyiwe kazi katika kukabiliana na majanga hapa nchini,”amesema.Kwa upande mwingine, amekipongeza chuo hicho kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutekeleza miradi mbalimbali ya Elimu ya Juu ambayo inalenga kuleta mageuzi ya kiuchumi.
Shahada hiyo imepokelewa na Mjane wa Marehemu Ningile Kapange baada ya mumewe Mwakatage kufariki kabla ya kutunukiwa shahada yake.

Waziri mkuu Majaliwa amesema utafiti wake una mahusiano makubwa na shughuli inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa katika kudhibiti maafa na majanga mbalimbali.
“Kwa kuwa ameshahitimu na leo anapata shahada na amefanya utafiti wa kina kwenye eneo la maafa na hasa majanga ya moto ambayo wakati wote serikali tumekuwa tukipambana nayo,
“Msomi wetu Marehemu Billy Mwakatage pamoja na utafiti ametoa mapendekezo mbalimbali, utafiti huu uchukuliwe na ufanyiwe kazi katika kukabiliana na majanga hapa nchini,”amesema.
Kwa upande mwingine, amekipongeza chuo hicho kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutekeleza miradi mbalimbali ya Elimu ya Juu ambayo inalenga kuleta mageuzi ya kiuchumi.

OUT kimepewa Sh. Bilioni 23 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi ambao unakwenda kuzalisha wataalamu wenye uwezo wa kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo, ufugaji na utalii ili kuongeza kasi ya Taifa letu kujikomboa kiuchumi.
Akizungumza katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la chuo, Profesa Joseph Kuzilwa, amesema chuo kimeendesha uchakataji wa mitaala na kuanzisha mitaala mipya ili kuendana na mabadiliko ya Sera ya Elimu ya 2014 iliyohuishwa 2023.
“Tunaishukuru sana serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo inahakikisha shughuli za chuo hiki hazikwami ili mazingira ya ufundishaji na kujifunza yaweze kuimarika, kuthibitisha hayo serikali imeipatia chuo majengo matano katika mikoa ya Lindi, Simiyu, Geita, Kigoma na Manyara,” amesema.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Carolyne Nombo, amesema chuo hicho kimekuwa na mchango mkubwa kwa nchi kwa kipindi chote cha miaka 30 ya utoaji wake wa huduma kwa kushiriki kutengeneza rasilimali watu ya Watanzania ambao wanaweza kutatua changamoto za nchi yetu.
“Chuo hiki kinatimiza miaka thelathini mwaka huu, wizara imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na chuo hiki katika miradi mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) wenye thamani ya shilingi bilioni 972.

Ambapo chuo hiki kimetengewa Sh. Bilioni 23 kwa ajili ya ujenzi wa maabara, kufanya mapitio ya mitaala, kusomesha wahadhiri na kuendesha program maalum za kuwapatia sifa wasichana wanaosoma masomo ya sayansi na wanaotoka katika.
Mazingira magumu kujiunga na elimu ya juu, lengo ni kupata rasilimali watu ya watanzania ambao ni makini na mahiri watakaoweza kutatua changomoto zinazowakabili wananchi na nchi yetu,” amesema.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Elifas Bisanda, amesema utaratibu wa kufanya mahafali katika mikoa mbalimbali una lengo la kuwataarifu wananchi kuwa chuo hiki kipo katika kila mkoa na ubora wa elimu yake umekubalika ndani na nje ya nchi.
Ameishukuru serikali kwa kuendelea kukiunga mkono chuo hicho kwa kukipatia fedha za maendeleo na miradi mbalimbali inayoendelea kukiimarisha.
Mahafali hayo ni ya 43 wahitimu wapatao 4307 wanahitimu katika kozi mbalimbali ambapo kati yao wahitimu 2070 ni wanawake sawa na asilimia 48.1 ukilinganisha na mahafali ya 42 yaliyofanyika Songea, Ruvuma ambapo wanawake walikuwa asilimia.44.