Na Lucy Lyatuu
WIZARA Ya Katiba Na Sheria imetoa huduma ya msaada Wa kisheria kwa watu zaidi ya 3500 katika maonesho ya biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba yaliyomalizika rasmuI juzi Dar es Salaam .
Aidha katika maonesho hayo Waziri Wa Wizara hiyo, Damas Ndumbaro amejumuika na wanasheria wengine Wa Wizara hiyo Kutoa huduma ya kisheria na kuchukuliwa hatua kwa wahitaji wengine.
Akizungumza,Waziri Ndumbaro amesema katika watu waliohudumiwa wanawake ni 1900 na wanaume ni 1630 na kwamba watalaam Wa Sheria wamekuwa wakishiriki vyema Kutoa huduma hiyo kwa wananchi.
Amesema katika maonesho hayo migogoro zaidi ya 500 imepatiwa utatuzi na inahusi masuala ya ardhi,mirathi,ndoa,ukatili Wa kijinsia na kesi za jinai na madai.
Amesema watendaji wanafanya majukumu yao kwa ufasaha wakiwa waametumwa na RAIS Samia Suluhu Hassan Kutoa huduma hiyo ya kisheria na wameonesha ukaribi kwa wananchi.
Amesema mbali na Wizara hiyo Kutoa huduma za kisheria lakini pia katika maonesho hayo zimekuwepo Ofisi nyingine zinazohusuka na mifumo ya utoaji haki,haki jinai na madai ikiwemo RITA,Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambaye anasimamia Uendeshaji WA kesi za madai dhidibya serikali.
Pia amesema katika maonesho hayo Ofisi ya mwanadheria Mkuu wa Serikali imetoa huduma,TUME Ya Haki Za Binadamu Na Utalawa Bora pamoja na Jeshi la Polisi.