Mwandishi wetu
ARUSHA: WAKULIMA wa mazao mbalimbali ikiwepo mbogamboga na matunda nchini, wametakiwa kutumia mbegu bora zinazoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi .
Hivi sasa Ongezeko la joto ardhini katika maeneo mengi nchini linalosababisha mbegu za mazao na mazao yaliyopandwa kuharibika na kushindwa kutoa mazao bora.
Mtaalam wa sayansi ya mimea wa kampuni ya Balton Tanzania, Chonya Wema akizungumza katika siku ya wakulima ya maonesho ya mbegu jijini Arusha, ambayo huandaliwa kila mwaka na kampuni hiyo, amesema kampuni hiyo imeanza kuzalisha mbegu zinazokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wema amewataka wakulima kutumia mbegu hizo kwa kuzingatia ushauri wa wataalam wa mimea ili kunufaika na kilimo na kuongeza uzalishaji.
Amesema hivi sasa kuna aina nyingi ya mbegu lakini baadhi ya hizo mbegu haziwezi kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa hivyo kushambuliwa na wadudu wa mimea kwa urahisi na kumpatia hasara mkulima.
“Kama ambavyo mnaona hili shamba darasa mazao yamekuwa vizuri kutokana na matumizi ya mbegu bora na pembejeo nzuri,” amesema.

Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya udhibiti wa mbolea ,Gothad Liampawe amesema, mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani ni kipindi cha kilimo .
Amesema mamlaka hiyo imejitahidi kudhibiti uingizwaji wa mbolea feki ili kumkwamua mkulima na athari za matumizi ya mbolea zisizo na ubora.
“Udhibiti wa mbolea uko vizuri kwani serikali imetoa ruzuku kwa mbolea ambapo mkulima aliyejisajili kwa ngazi ya Kijiji anapatiwa mbolea ya ruzuku,” amesema.

Baadhi ya wakulima na wauzaji wa pembejeo wakizungumza katika maonesho hayo walipongeza a kampuni ya BALTON Tanzania ambao ni waagizaji na wasambazaji wa mbegu nchini.
Saidi Bakari Hamza kutoka Pemba na Masudi Salimu Nasoro kutoka Unguja wamesema wamejifunza kutambua mbegu bora kulingana na maeneo waliyotoka na kuahidi kwenda kutoa ushauri kwa wakulima wa maeneo yao.
‘’Kumekua na changamoto kwa wakulima tunaowahudumia kule pemba pindi unapowauzia mbegu waliyohitaji

Meneja mkuu wa kampuni ya Balton Tanzania Jacob vorster amesema waliamua kuwaita wakulima hao na wasambaji wa mbegu katika mafunzo hayo ili kuongeza ujuzi wa mbegu na kilimo.
Amesema wanataka kuona kilimo.ambacho kina tija katika maeneo yao na kufanikisha malengo ya mkulima kupata mazao mengi na bora baada ya kutumia mbegu bora.
Amesema kufanya kilimo chenye tija katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi kutapelekea nchi kuwa na chakula cha kutosha na pia kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja.

Awali akifungua maonesho hayo,Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu nchini (TASTA) Bobu Shuma amewataka wakulima na wauzaji mbegu kushirikiana.
Amesema wakulima wanatakiwa kupata ushauri wa mbegu bora inayofaa kulingana na mahali wanapolima kuendana na mazingira ya hali ya hewa.
“Lazima wauzaji ña mbegu mshirikiane na wakulima ili muwasaidie kupata mazao bora na kuepuka hasara ya kutumia mbegu zisizo na ubora,” amesema.
Wakulima na mawakala.wa pembejeo zaidi ya 400 wameshiriki katika maonesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka.