MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wanaodaiwa Kumuua Ofisa TRA Washikiliwa na Polisi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wanaodaiwa Kumuua Ofisa TRA Washikiliwa na Polisi
Habari

Wanaodaiwa Kumuua Ofisa TRA Washikiliwa na Polisi

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WATUHUMIWA wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, kwa tuhuma za kufanya mauaji ya mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), aitwaye Amani Simbayao ikiwa ni pamoja na kumjeruhi Adriano Fredrick wa mamlaka hiyo.
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Muliro ametaja watuhumiwa hao kuwa ni Deogratius Masawe (49) na Idd Bakari (30) wote wanafanya kazi ya ukuli wakazi wa Tegeta kwa Ndevu.
Wengine ni mpiga debe Omar Issa (47), mkazi wa Tegeta Dawasco na Rashid Mtongma (29) mwendesha Bodaboda mkazi wa Bunju.

Amesema watuhumiwa hao na wengine ambao bado wanahojiwa kwa kina walikamatwa baada ya kuwashambulia maofisa hao wa TRA wakati wakitekeleza majukumu yao ya kisheria.
“Waliliharibu pia gari namba STL 9923 aina Toyota Land Cruiser Hardtop nyeupe mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,” amesema.
Tukio hilo limetokea Disemba tano, 2024 majira ya saa tatu usiku eneo la Tegeta kwa Ndevu Kinondoni baada ya Maofisa hao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kukamata gari namba T 529 DHZ aina ya BMW rangi nyeupe lililodaiwa kuwa na makosa ya kikodi.
“Jeshi la Polisi Kanda maaalum ya Dar es Salaam linawaonya vikali na halitavumilia watu ambao wanataka kujenga tabia ya kuwashambulia watumishi wa Serikali wakati wakitekeleza majukumu yao licha ya kuwa wanakuwa wamefuata taratibu zote za kisheria,” amesema.
Amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika kwa kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za kisheria.

You Might Also Like

Wafanyakazi waitwa kupeleka changamoto za kikazi CMA

Bodi ya Bima ya Amana Yatoa  Bil 9.07 , Fidia Kwa Wateja Wa Benki Saba   Zilizofilisika

Mfumo Wa Kuwabana Wachafuzi Wa Choo umetengenezwa

Hivi Ndivyo Vipaumbele Vya Maliasili

UDSM Yaja Na Bajaji Inayotumia Maji Na Mafuta

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Nguvu Zaidi Iongezwe Kwenye Tafiti Zinazogusa Maisha Ya Jamii
Next Article Watumishi REA Watakiwa Kufanya Kazi Kuendana Na Kasi Ya Serikali
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Aituza UDSM kwa Kuongoza Eneo La Elimu, Utafiti, Ubunifu Sabasaba 2025
Habari July 14, 2025
Nyanya Cheri na Ngogwe Chungu Zarejea 
Habari July 13, 2025
NFRA Yawaalika Wadau Kununua Nafaka kwa Masoko ya Ndani na Nje
Habari July 13, 2025
Kafulila: Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma Kuboresha Huduma
Habari July 13, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?