Na Lucy Lyatuu
JUKWAA La Watumiaji Tanzania (TCF) limesema wataka wananchi kuchukua hatua iwapo watapata huduma ambayo haijakidhi viwango husika na kutoridhisha.
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo,Daud Daud amesema hayo Dares Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya siku ya haki za mtumiaji duniani ambazo hufanyika kila mwaka Machi 15.
Amesema mtumiaji wa anapaswa kuwa na nguvu ya kufanya maamuzi sahihi kwa kupata huduma salama,nafuu na endelevu.
“Kila mtu ana haki ya kuishi katika jamii inayowajibika kulinda mazingira na rasilimali kwa vizazi vijavyo,” amesema nakuongeza kuwa hatua ya kwanza ambayo mwananchi anapaswa kujua ni kuwasiliana na mtoa huduma.
Amesema iwapo mtoa huduma hakutoa majibu ama maelekezo yanayoridhisha hapo mtumiaji anapaswa kuwasiliana na mdhibiti za huduma ikiwa ni Pamoja na kuwasilisha nyaraka zozote alizofikisha kwa mtoa huduma.
Kuhusu maadhimisho hayo amesema kwa mwaka 2025 maadhimisho yatafanyika mkoani Morogoro ikibebwa na kauli mbiu ya Haki na Maisha Endelevu kwa Mtumiaji.
Amesema maadhimisho hayo yanakusudia kuhamasisha matumizi salama na endelevu ya rasilimali huku yakitoa jukwaa la majadiliano kati ya watumiaji, watoa huduma na wadau wa maendeleo.
Amesema Jukwaa hilo kwa kushirikiana na The Foundation For Civil Society (FCS) linaadhimisha siku hiyo ikiw a na lengo la kulinda haki za watumiaji n a kuhimiza matumizi salama na endelevu ya huduma, hiyo ni fursa ya pekee kwa wananchi kupata elimu kuhusu haki zao.
Amesema katika maadhimisho hayo TCF inahimiza matumizi salama ya huduma katika sekta za nishati,mawasiliano na usafiri wa ang ana nchi kavu, serikali inalenga kuhakikisha kuwa ifikapo 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.
Daud amesema kwa upande wa mawasiliano, usalama wa mtumiaji mtandaoni ni ajenda muhimu mwaka 2025 ambapo inahimiza ulinzi wa faragha n a matumizi salama ya huduma za kidigitali, pia usalama katika sekta ya usafiri wa ang ana nchi kavu utaangazwa ili kuwa na huduma bora kwa watumiaji.
Kwa upande wake Ofisa Mawasiliano wa FCS Sarah Masenga amesema wameshirikiana na Jukwaa hilo ili kuongeza uelewa kwa waanchi kuhusu huduma wanazozipata na sehemu wanayotakiwa kupeleka malalamiko yao.
Jukwaa la watumiaji linajumuisha mabaraza ya kutetea watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa ambayo ni LATRA-CCC, TCAA -CCC,EWURA-CCC NA TCRA-CCC.