MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wananchi wa Bukoba Wapewa Vizimba vya Samaki Kuongeza Mapato
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wananchi wa Bukoba Wapewa Vizimba vya Samaki Kuongeza Mapato
Habari

Wananchi wa Bukoba Wapewa Vizimba vya Samaki Kuongeza Mapato

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Bukoba Vijijini, Dkt. Jasson Rweikiza, ameuliza katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma: “Je, lini wananchi wa Bukoba watawezeshwa kwa kupewa vizimba vingi zaidi vya samaki ili kushiriki katika kukuza uchumi?”
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ng’wasi Kamani amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake, kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), inaendelea na zoezi la utoaji wa mikopo ya masharti nafuu kwa ajili ya vizimba, vifaranga na chakula cha samaki.
Amesena katika awamu ya kwanza, mikopo ya vizimba 44  ikijumuisha vizimba 30 Bukoba, 12 Muleba na viwili Misenyi  yenye thamani ya Sh. 986.80 milioni ilitolewa mkoani Kagera kwa wanufaika 101.
Alisema zaidi kwamba katika mwaka wa fedha 2025/2026, Wizara imepokea kiasi cha Sh. bilioni 7 kutoka Hazina kwa ajili ya kuwezesha vijana kupata mitaji kupitia mikopo yenye masharti nafuu.
Amesema fedha hizo zitatumika kukopesha vijana 308 waliohitimu mafunzo, wakiwemo vijana 32 kutoka Mkoa wa Kagera.
Aidha, Wizara inatarajia kupokea sehemu ya Sh. bilioni 200 ambazo ni ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100, zitakazoelekezwa katika kuwezesha mikopo ya vizimba.
Wizara pia inaendelea kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuendelea kutoa mikopo ya vizimba katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kwa vijana wa Bukoba.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Kamani, ameongeza kwamba Serikali inahimiza Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mikopo yao kwa shughuli za ufugaji samaki iwapo kuna maeneo yanayofaa kwa shughuli hiyo, ili kuongeza uwekezaji wa vizimba na fursa za ajira kwa wananchi.

You Might Also Like

NIC Yatoa Elimu ya Bima Kwenye Kijiji cha Bima, Maonesho ya Madini Geita

China Yafundisha Wanafunzi DIT kuzifikia fursa

Dira za Maji Kumaliza Kero ya Ankara

Utekelezaji Mradi Mkubwa Wa Maji Mwanza Wafikia Asilimia 35

TASU yaiomba serikali inunue kutoa ajira kwa mabaharia

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yaanza Mchakato wa Kujenga Uwanja wa Ndege Kyabajwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yaanza Mchakato wa Kujenga Uwanja wa Ndege Kyabajwa
Habari February 4, 2026
Katoro Yapata Gari Jipya la Zimamoto, Kuwasili Februari 9
Habari February 4, 2026
Waziri Mbarawa Aagiza Adhabu Kali kwa Madereva, Makondakta Wanaonyanyasa Wanafunzi
Habari February 4, 2026
Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?