Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Balozi Aisha Amour ameupongeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kusaidia program ya Wahandisi wataraji wapatao 428 kote nchini ili kupata mafunzo ya kuwajengezea uwezo ili kukuza tasnia yao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya 21 ya siku ya Wahandisi nchini yanayofanyika Dar es salaam Balozi Amour amesema TARURA inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahandisi wataraji wapatao 428 wakifuatiwa na TANROADS (251),TTCL(164), RUWASA (156) na TANESCO (126).
“Naipongeza sana TARURA ni Taasisi inayoongoza kwa kuwapokea wanafunzi wengi wanokuwa katika program hii, tatafurahi na Taasisi nyingine nazo kujitokeza”, amesisitiza Katibu Mkuu