Lucy Lyatuu
BOdi Ya Usajili Wabunifu Majengo Na Wakadiriaji Majenzi Nchini ( AQRB) imesema kwa mwaka 2025 wapo waendelezaji Majengo 103 ambao kesi zao ziko mahalamani kwa kushindwa kutumia watalaam waliosajiliwa na Bodi.
Kaimu Msajili Wa Bodi, Daniel Matondo amesema hayo katika Banda la Bodi hio lililoko katika maoneshobya 49 Ya Kimaraifa Ya Biashara maarufu kama sabasaba yanayoendelea Dar es Salaam.
Amesema kimsingi uendelezaji Wa Majengo kama ya makanisa, viwanja vya michezo na stoo kubwa za kuhifadhia mizigo vyote vinahitaji Wabunifu na Wakadiriaji.
“Hivyo kama unaendeleza jengo la aina hio hakikisha unawasiliana na bodi Ili usikumbwe na tatizo na Kila mwaka tunadhibiti Ili watalaam wafanye kazi Yao kwa weledi,” amesema.

Amesema wapo watalaam wanaotozwa faini,kufutwa kabisa na wengine kusimamishwa pindi wanapofanya kazi kinyume na miongozo inayowaongoza.
Aidha amewakaribisha wananchi kufika katika Banda lao katika maonesho hayo Ili Kupata elimu nab Kujifunza zaidi kujua hasara na faida za kutumia Bodi”Watu wafike kwenye maonesho ya sabasaba kujua majukumu ya Bodi pamoja na huduma wanazotoa,” amesema na kuongeza kuwa Bodi Iko kisheria ambapo inafanya kazi Kudhibiti taaluma hio.
Aidha amesema licha ya kuwepo kwa Bodi hiyo wapi waendelezaji Majengo wanaojenga pasipo kutumia watalaam licha ya kwamba Sheria inaelekeza lazima ujenzi. Wa jengo lolote la gorofa kuhusisha mtaalam aliyesajiliwaa na Bodi.
