Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 17

Waandishi Watakiwa Kuandika Habari Za Uchunguzi Juu Ya Athari Za Mabadiliko Ya Tabia Nchi Ili Kuleta Uwajibikaji

Na Lucy Lyatuu, Dodoma
WAANDISHI  wa habari za mazingira nchini, wametakiwa kuandika kwa kina habari za uchunguzi juu ya mambo yanayoendelea nchini ambayo yanachangia  athari za mabadiliko ya tabia nchini ili kuokoa jamii.
Maeneo mengi nchini, yanaendelea kuathirika na athari ya mabadiliko ya tabia nchi, kutokana na kuendelea ukataji wa miti, upanuzi wa mashamba maeneo yaliyohifadhiwa, uvamizi wa vyanzo vya maji, uchafu wa mazingira, uvamizi wa maeneo ya nyanda za malisho na uchimbaji madini ambayo haujali athari za kimazingira.
Habari Picha 13790
Mhariri  mwandamizi wa habari za mazingira, Deodatus  Mfugale akitoa mada ya habari za  uchunguzi wa mazingira, katika mafunzo ya wanahabari 35 wa mikoa ya kanda ya kati, jijini Dodoma, mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu(THRDC) na Taasisi ya Wanahabari ya Usaidizi wa Jamii za Pembezoni(MAIPAC) kwa udhamini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO).
Mfugale alisema,Wanahabari wana nafasi ya kuokoa jamii juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchini, kwa kuandika na kuibua mambo ambayo yanachochea uharibifu wa mazingira kwa kutumia kwa usahihi na kutumia takwimu sahihi, sheria na hivyo kuibua uwajibikaji .
“Waandishi nendeni mkaandike habari za uchunguzi kusaidia jamii ili kuifanya dunia kuendelea kuwa salama lakini muandike kwa usahihi  na kujumuisha sauti za wananchi wanaoathirika”anasema.
Habari Picha 13791
Mkurugenzi mtendaji wa MAIPAC, Mussa Juma akitoa mada ya msingi wa habari za mazingira alisema mwandishi wa habari za mazingira  anapaswa kuandika kwa usahihi,kuandika kwa uhuru,kuelewa maudhui ya jambo ambalo anataka kuliandika, kushirikisha sauti za makundi yote katika jamii ikiwepo Wanawake, vijana, kuleta uwajibikaji na kutetea maslahi ya umma.
Juma alisema wanahabari wanapaswa kuchunguza zaidi athari za mabadiliko ya tabia nchi, katika maeneo mbalimbali, ambazo zimetokana na ongezeko la joto duniani,Ukame, Mafuriko,upungufu wa uzalishaji wa chakula,uharibifu wa ikolojia.
Habari Picha 13792
Naye Mkurugenzi wa Mkurugenzi  wa Miradi na Uendeshaji wa (THRDC), Wakili Halima Sonda akizungumzia Ukatili dhidi ya waandishi wa habari wanawake, alitaka wanahabari wanawake wapewe fursa sawa na waume katika kuandika habari za uchunguzi za mazingira.
Hata hivyo, alisema kumekuwep udhalilishaji wa wanawake mitandaoni,mifumo dume katika jamii mambo ambayo yanapaswa kupingwa kwani tayari kuna sheria kadhaa, zinazopinga ukatili dhidi ya wanawake na wanahabari wanawake wa mazingira wanapaswa kuzijua .
Habari Picha 13793
Habari Picha 13794
Mafunzo hayo kwa waandishi kanda ya Kati, kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa, Morogoro ni mfululizo wa mafunzo yanayotolewa na THRDC na MAIPAC kwa wanahabari nchini kupitia mradi wa  kuwezesha waandishi wa habari za mazingira kuimarisha uwezo wa wanahabari ili kuchangia uwajibikaji  wa mazingira na kukuza uelewa katika jamii tayari mafunzo yametolewa kanda ya kaskazini na Kanda ya Ziwa.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.