MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: VETA Mtwara Watua Na Mwani Maadhimishilo Ya Miaka 30
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > VETA Mtwara Watua Na Mwani Maadhimishilo Ya Miaka 30
Habari

VETA Mtwara Watua Na Mwani Maadhimishilo Ya Miaka 30

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
– Wasema Unarekebisha Nguvu Za Kiume, Kupunguza Uwezekano Wa Kupata Tezi Dume

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: MTAALAMU wa Fani ya Maabara katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), kilichopo Mtwara, Oliver Mbemba ameuelezea mwani kama zao bahari linalosaidia kwenye mfumo wa uzazi kwa wanaume na wanawake.
Kwa wanaume amesema zao hilo la  mwani linarekebisha nguvu za kiume, ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezekano wa kupata tezi dume.
Mbemba amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya miaka 30 ya uanzishwaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ( VETA), yanayoendelea Katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam (JNICC).
Akizungumza kwenye Banda la Maonesho la VETA Mtwara, amesema kwa wanawake inasaidia kurekebisha uiano wa homoni na kuondoa maumivu wakati wa hedhi.
“Pia linasaidia wamama wanaonyonyesha kwenye uzalishaji wa maziwa,” amesema.
Amesema zao bahari hilo lina madini 92 ambayo hufanya kazi mbalimbali katika mwili ikiwemo pia utunzaji wa ngozi, mfumo wa mzunguko wa damu mwilini kwani huweza kurekebisha shinikizo la juu la juu, na shinikizo la chini la damu.
Amesema chuo hicho wamekuwa wakifanya tafiti kwenye udongo na mazao bahari ambayo ni mwani, lakini pia maji salama yanayotumika hospitalini.
” Ni fani kamili mwanafunzi anasoma mwaka wa kwanza mpaka wa tatu, akimaliza atafanya kazi kiwanda chochote,” amesema.
Amesema pia wana bidhaa mbalimbali za mwani ikiwemo unga wake ambao hutumika kwenye chakula, sabuni za kuogea, mafuta ya maji na mgando.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore amesema wataendelea kutoa elimu ya ufundi stadi pamoja na kusimamia bunifu na teknolojia mbalimbali.

You Might Also Like

TAMWA Yawawezesha Wanawake Kupitia Mradi wa Nyuki

VETA Shinyanga Yatumia Kompyuta Kubuni Bidhaa 

Dkt Biteko Ampongeza Mwanafunzi Aliyeelezea Miradi Ya Umeme

Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Kwenye Kilele Cha Siku Ya Utumishi Wa Umma

Spika Ahoji Mwongozo Wa Wanaojitolea Kazin

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tanzania Ina Utolevu Wa Chakula Kwa Miaka Minne Uongozi Wa Samia
Next Article VETA Mikumi Yatengeneza Mashine Ya Kuchakata Majani Ya Mifugo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vita Mashariki ya Kati Vyatikisa Uchumi wa SADC, Mawaziri Watakiwa Kuchukua Hatua
Habari March 12, 2026
Mamlaka Za Mitaa Ondoeni Urasimu Katika Kuanzisha Biashara Mpya-Waziri Mkuu
Habari March 12, 2026
Ofisi Ya Taifa Ya Takwimu  Kufanya Tafiti Kwa Wakala Wa Huduma Za Fedha,Viwandani
Habari March 12, 2026
GCLA  Yanunua Mitambo Mikubwa Inayogharimu Sh Bil 32.25 Kuimarisha Uchunguzi Wa Sampuli
Habari March 12, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?