MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Uwekezaji wa NSSF wa Mzizima Towers Kufungua Fursa Mpya za Biashara na Utalii Dar
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Uwekezaji wa NSSF wa Mzizima Towers Kufungua Fursa Mpya za Biashara na Utalii Dar
Habari

Uwekezaji wa NSSF wa Mzizima Towers Kufungua Fursa Mpya za Biashara na Utalii Dar

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Yafikia Asilimia 91, Kukamilika Desemba 2026
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM: SERIKALI imesema mradi wa uwekezaji wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi la Mzizima Towers unaotekelezwa jijini Dar es Salaam na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umefikia asilimia 91 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo Desemba 31, 2026.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, alipowasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi huo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Habari Picha 11524
Kwa mujibu wa Waziri Sangu, mradi huo wa uwekezaji unahusisha ujenzi wa minara miwili, ikiwemo mnara wa biashara wenye ghorofa 35 na mnara wa makazi wenye ghorofa 32, ukiwa na jumla ya eneo la ujenzi la mita za mraba 95,018.15.
Amesema majengo hayo yamebuniwa kwa kuzingatia viwango vya kisasa vya usanifu wa kimataifa ili kukidhi mahitaji ya biashara, makazi na huduma za utalii katika jiji la Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utakuwa na hoteli ya hadhi ya nyota tano itakayoendeshwa na Radisson Hotel Group, yenye jumla ya vyumba 156 vya kulala pamoja na vyumba 132 vya makazi ya muda mfupi.
Sangu amesema mradi huo unatekelezwa kwa asilimia 100 na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kama sehemu ya mkakati wa Mfuko huo kuwekeza katika miradi mikubwa ya kimkakati yenye tija kwa wanachama na taifa kwa ujumla.
Amebainisha kuwa uwekezaji huo unalenga kuongeza thamani ya mali za Mfuko pamoja na kuimarisha uwezo wake wa kulipa mafao kwa wanachama.
Habari Picha 11525
Akizungumza baada ya ziara ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii,  Hawa Chakoma, amesema wajumbe wa kamati wanamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua mradi huo uendelee kutekelezwa ili uweze kuleta tija kwa Mfuko na Taifa kwa ujumla.
“Sisi kamati tumefika hapa na kujionea kazi inayofanyika katika mradi huu. Kazi ni nzuri sana na inaonesha kuwa uongozi wa NSSF chini ya Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba, umekuwa mfano wa kuigwa katika usimamizi wa miradi,” amesema Hawa.
Habari Picha 11526
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa kufanya ziara ya kikazi na kujionea maendeleo yaliyofikiwa katika mradi huo.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Kafiti Kafiti wameipongeza NSSF kwa uwekezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla.
Naye Kangi Lugola amesema mradi wa Mzizima Towers ni uwekezaji muhimu wenye tija kubwa kwa Mfuko na Taifa kwa ujumla, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kwa usimamizi mzuri wa Mfuko na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Habari Picha 11523
Habari Picha 11522
Habari Picha 11527
Habari Picha 11528
Habari Picha 11529
Habari Picha 11530

 

You Might Also Like

Polisi Yatoa Onyo Kali Kwa Waganga wa Tiba Mbadala

Chalamila Akabidhi milioni 100, saruji Kukamilisha Zahanati

TPHPA Yaleta Mapinduzi Mapya Katika Kilimo Kupitia Teknolojia ya Vinasaba

Halmashauri Zahimizwa Kujenga Viwanda Vya Michezo.

TMDA Kudhibiti Bidhaa Za Tumbaku Ili Wananchi Wasiendelee Kupata Madhara

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Sh. Bilioni 883.93 Zatumika Kutekeleza Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira
Next Article Walimu Ni Nguzo ya Maadili na Uzalendo kwa Taifa – Rais CWT
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tanzania Yajikita Katika Ushirikiano wa Kikanda Kuhusu Maji
Habari March 25, 2026
TPHPA Yazidisha Ulinzi wa Mazao, Kudhibiti Magonjwa ya Viazi, Funza Weupe
Habari March 25, 2026
Katibu Mkuu Mwajuma Atunukiwa Tuzo, Ahimiza Mshikamano Sekta ya Maji
Habari March 24, 2026
Dkt. Nchimbi Azindua Mfumo Mpya wa Utabiri wa Kiasi cha Maji Morogoro
Habari March 23, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?