Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: Usajili mashauri kwa njia ya mtandao, umesaidia kuharakisha ufunguaji wa mashauri katika mahakama.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Salma Maghimbi amesema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini Kanda ya Dar es Salaam.
Maghimbi amesema kwa kuharakisha ufunguaji wa mashauri, matokeo yake hupelekwa mahakamani kwa wakati, kusajiliwa na kupangiwa Jaji au Hakimu ndani ya saa chache.

Kwa upande mwingine amesema hatua kubwa imepigwa katika uteuzi wa majaji wa mahakama Rufani na mahakama Kuu, mahakimu pamoja na kuajiri watumishi wengine wa kada mbalimbali.
“Vile vile mahakama imeendelea kupunguza mlundikano wa mashauri katika ngazi zote za mahakama, na kuongezeka kwa imani ya wananchi na wadau kwa mahakama,” amesema.

Amesema wakati wa kuanza naboresho mwaka 2015 mpaka mwaka 2023, tafiti zilionyesha kuwa imani ya wananchi kwa mahakama imeongezeka kutoka asilimia 61 mwaka 2015 hadi asilimia 88 mwaka 2023.