Na Lucy Lyatuu
CHUO Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kimepokea tuzo ya mshindi kwa makundi ya vyuo vikuu katika maoneshobya 49 ya Biashara maarufu kama sabasaba ikiwa ni kutokana na jitijada zake za kuwa na tafiti pamoja na bunifu mbalimbali.
Akizungumza baada ya kupokea Tuzo hiyo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Wa UDOM Profesa Razack Lokina amesema katika maonesho hayo kazi nzuri imefanywa ambazo zimevutia wananchi wengi.
Amesema katika maonesho hayo wamekuwa na bunifu na tafiti wakitoa huduma za Tiba,Sheria, kupima afya na wanajivunia kuwa na watalaam katika maoneshob hayo.
,”Siri Ya mafanikio hadi Chuo cheti kushinda ni kufanya maandalizi mapema,Chuo cheti ni kikubwa na lazima muonekano wetu uangaze ule ukubwa Wa Chuo,” amesema Profesa Kilokina.
Amesema zipo bunifu nyingi zimefanyika na katika maonesho hayo Wamekuja na bunifu za kisayansi za roketi lakini Kuna dawa lishe, na miradi mingi ya uwekezaji imeoneshwa katika maonesho hayo pamoja na namna ya kubadilishabtaka za plastiki kuwa mkaa safi na Kutoa ushauri kwenye Sheria,Tiba na mambo mengine ya afya.
Hata hivyo anawakaribisha wazazi kupeleka watoto wao kusoma katika Chuo hicho ambacho dirisha la udahili linafungulia kuanzia Julia 15,2025 kwani Kuna program mbalimbali ikiwemo Tiba,famasia,biashara ,Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ,(TEHAMA) na uinjinia.