Na Lucy Ngowi
PWANI: CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania ( TUGHE), kimetoa zaidi ya Sh. Bilioni tatu mwaka jana 2024, kama zawadi kwa wafanyakazi hodari.
Aidha kwa mwaka huu 2025, TUGHE inatarajia kujenga jengo lenye thamani ya takribani Sh. Bilioni 10 likiwa na ofisi za Makao Makuu TUGHE, Hotels na Kumbi za mikutano.
Katibu Mkuu TUGHE ambaye ni Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA), Hery Mkunda amesema hayo alipozungumza na Mwandishi wa Habari wa Mfanyakazi Tanzania.
Mkunda amesema, ” Katika mwaka 2024 tumepata wafanyakazi hodari wengi ukilinganisha na mwaka uliopita 2023.
“Wafanyakazi hodari peke yake katika mwaka 2024 nchi nzima wamepata zawadi zaidi ya Sh. Bilioni tatu,”.
Mkunda amesema wafanyakazi hao wamekitangaza chama vizuri.
Kuhusu ujenzi wa jengo hilo linalogharimu Sh. Bilioni 10, amesema tayari wameshasaini mkataba na mkandarasi ambaye ataanza ujenzi muda wowote kuanzia sasa.
Amesema jengo hilo linajengwa Dodoma, litajengwa ndani ya miezi 18, litakuwa na ghorofa nane.
Mkunda pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika Mashariki, pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Duniani