Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) wamefanya mazungumzo wakiwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwan Kikwete Jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, pamoja na mambo mengine walipata nafasi ya kujadili masuala mbalimbali ya Wafanyakazi ikiwemo utekekezaji wa ahadi ya Serikali kuhusu nyongeza ya siku za likizo ya Uzazi kwa wafanyakazi wanaojifungua watoto njiti kama ambavyo ilitangazwa na Makamu wa Rais,. Dkt. Philip Mpango.
Dkt Mpango alitangaza hivyo alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi 2024 Kitaifa Jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa TUGHE ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUCTA, Hery Mkunda amemweleza Waziri huyo changamoto mbalimbali wanazopata wafanyakazi wanaojifungua watoto njiti ikiwemo kukosa haki zao muhimu katika maeneo yao ya kazi na kukosa muda wa kuwahudumia watoto hao.
Pia alimwomba waziri kulichukua suala hilo na kulipeleka katika hatua zinazofuata ili kuwezesha kutatua changamoto hizo.
Kwa upande wake Waziri Kikwete ameahidi kulifanyia kazi suala hilo kama ambavyo Viongozi hao wameliwasilisha kuhakikisha linafanyika na kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia ni maelekezo kutoka kwa mamlaka ili kuleta motisha kulinda Afya ya mama na mtoto.
Naye Mkurugenzi wa DMF, Doris Mollel ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na wadau katika kutekeleza Ajenda ya masuala ya Watoto njiti na kubainisha kuwa Taasisi yao imekuwa ikipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali kuhusu kukosa haki zao wanapojifungua.
Hivyo ameiomba seeikali kusaidia utatuzi wa changamoto kwa kusimamia kupitishwa kwa sheria hiyo.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Zuhura Yunusi, Kaimu Naibu Mkuu wa TUCTA Said Wamba, Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE, Rugemalira Rutatina