Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA La Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua kifurushi cha huduma ya faiba mlangoni maarufu kama T’ Fiber Triple Hub ambacho kinajumuisha huduma tatu muhimu yaani mfumo wa kifurushi kimoja, bili moja huduma tatu.
Meneja Masoko wa TTCL, Janeth Maeda amezindua kifurushi hicho Dar es Salaam an kuongeza kuwa jitihda hizo ni kwa Shirika hilo kuendelea kuwekeza zaidi katika kuhakikisha huduma za mawasiliano nchini zinakuwa imara za uhakika na kwa gharama nafuu.

Limesema kupitia uwekezaji huo linalenga kufikisha huduma za kisasa hadi katika makazi ya watu, katika ofisi na hata katika biashara kwa kuwaunganisha watanzania wote bila kujali walipo.
Amesema TTCL imeendelea kusikiliza kwa makini maoni, mahitaji na matarajio ya watanzania kutoka kila upande wa nchi ya Tanzania.
“Tumejifunza kwamba wananchi wanahitaji huduma rahisi kutumia gharama nafuu lakini zenye ubora wa juu itakayotoa tafsiri ya thamani halisi kwa fedha wanazotumia katika harakati za kuboresha maisha yao, ” amesema.

Kuhusu kifurushi hicho amesema kinajumuisha huduma tatu muhimu yaani mfumo wa kifurushi kimoja, bili moja huduma tatu.
Amesema kifurushi kinajumuisha huduma tatu muhimu yaani intanenti kwa matumizi ya familia, ofisi, biashara na hata mifumo ya kidigitali.
Vilevile amesema kifurushi kinajumuisha huduma ya simu ya mezani inayompa mteja fursa ya kupiga au kupokea simu kwa urahisi kupitia miundombinu ya faiba na pia kinajuisha huduma ya intanent na dakika kwa simu ya mkononi inayomuwezesha mteja kupata vifurushi vyenye GB na dakika za kutosha ambayo vinaweza kutumika popote pale mteja alipo akiwa na lainibya simu ya TTCL na anaweza kuwaunganisha ndugu na jamaa au wafanyakazi wake na kufurahia kasi ileile.

Maeda amesema kifurushi ni suluhisho kamili nyumbani. Ofisini au biashara, kimeundwa ili kurahisisha maisha, kupunguza gharama na kutoa thamani kubwa zaidi kwa wateja.
Amezitaja faida za kifurushi hicho kuwa ni ni kifurushi kwa wateja wote wapya na waliopo wanaweza kufurahia huduma hiyo na ni kifurushi rahisi chenye huduma zote tatu zikipatikana kwenye kifurushi kimoja, bili moja ukipata huduma tatu popote.
Amesema kifurushi kina ubora na uhakika kwa saa 24 na kinapatikana kwa sh 70,000 kikiwa na intanet ya kasi kubwa bila kikomo yenye uwezo wa hadi 20 Mbps upload na 20 Mbps download, intenet inayokidhi mahitaji ya nyumbani, kazini na kwenye biashara.


