Na Mwandishi Wetu
MAREKANI: Donald Trump anarejea madarakani baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Marekani uliofanyika Novemba nne, mwaka huu 2024.
Trump anarejea madarakani ikiwa miaka minne imepita tangu aliposhindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, uliomuingiza madarakani Rais Joe Biden, anayemaliza muda wake.
Matokeo yanaonyesha kuwa, hadi mchana wa Novemba sita, 2024 Trump alikuwa amepata kura milioni 71 sawa na asilimia 51 ya kura zote zilizohesabiwa huku mpinzani wake Kamala Harris amepata kura milioni 65 sawa na asilimia 47.