Na Danson Kaijage
SERIKALI imetoa kiasi cha SH. Trioni 1.2 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji na kuanzisha mipya katika Jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA),Mkama Bwire amesema hayo wakatii akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Amesema pia serikali imetoa Sh. Bilioni 16 kwa ajili ya kubadilisha miundombinu mitambo ya maji ambayo imechakaa.
Katika kutekeleza miradi ya maendeleo, Bwire amesema Serikali imetoa kiasi cha Sh. Bilioni 35.6 kwa ajili ya ujenzi wa tenki kubwa la maji sehemu ya Bangulo kwa ajili ya kupunguza changamoto ya maji.
Amesema ufungaji wa dira za aina ya lipa kabla ya matumizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa cha malimbikozo ya mademi kwa wateja wa majumbani na taasisi za Umma.
Bwire amesema mamlaka hiyo kwa sasa inatarajia kufunga Dira 65,000 katika Jiji la Dar Es Salaam na kwa kufunga dira hizo zitapunguza malimbikizo ya madeni kwa wateja au malalamiko ya kubambikiwa bili.
Amesema ufungaji wa dira hizo za lipa kabla ya kutumia zitawafanya wateja wengi kutumia maji yao kadri ya mahitaji kama ilivyo kwa Shirika la Umeme nchini Tanesco