Na Lucy Ngowi
CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), kinapigania Mkataba wa Hali Bora za Kazi kwa Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kwa miaka 11 sasa.
Naibu Katibu Mkuu wa TRAWU, Edo Makata amesema hayo alipozungumza na Gazeti la Mfanyakazi.
Malola amesema tokea 2013 TRC ilipovunja mkataba na wafanyakazi wake kutokana na sababu za kisheria, kesi iliendeshwa mahakamani mpaka 2020 ambapo mwajiri alitakiwa kukaa nao ili kutengeneza mkataba.
“Tumeanza mazungumzo na tayari tunayo nakala ya kuanzia mahali ambapo tunaweza tukaingia mkataba, na tayari tupo kwenye hatua fulani upande wa serikali na mazungumzo yanaendelea.
“Tunaamini kwamba mkataba wa hali bora unaweza kufikiwa kwa wafanyakazi wa TRC lakini imekuwa ni changamoto kubwa,” amesema.
Amesema upande wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), suala la mkataba na hali bora limekuwa likizingatiwa kwa wakati.