Na Lucy Lyatuu
RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na Namibia zimekubaliana kuongeza juhudi za kukuza ushirikiano wa kiuchumi kwa kutafuta njia madhubuti za kukuza biashara baina yao, ikiwa ni Pamoja na kuwezesha uwepo wa miradi mikubwa ya uwekezaji kutoka pande zote mbili
Wakizungumza na vyombo vya habari akiwa na Rais wa Namibia Dk Netumbo Nandi-Ndaitwa mara baada ya mazungumzo rasmi, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kuchochea ajira kwa vijana na kupunguza umaskini.
Aidha marais hao wameeleza dhamira ya kupanua ushirikiano katika maeneo ya elimu, utalii, mazingira, mifugo, uvuvi na nishati na kuweka msisitizo kwa sekta binafsi kuwekeza kwa kiwango kikubwa tofauti na hali ilivyo sasa.
Rais Samia amebainisha kuwa biashara kati ya Tanzania an Namibia imeongezeka kutoka sh bilioni 17 hadi bilioni 20 kati yam waka 2019 na 2023 hata hivyo amesema kiwango hicho bado ni kidogo kulinganisha na fursa zilizopo na kuwataka wafanyabiashara wan chi hizo mbili kuchangamkia fursa hizo.
Kadhalika ameikaribisha sekta binafsi ya Namibia kuja kuwekeza na kushirikiana na Tanzania katika sekta za uongezaji thamani wa mifugo,uvuvi na katika sekya utalii
Katika eneo la utamaduni Rais Samia ameeleza kuwa Tanzania na Namibia zinatarajia kushirikiana katika sekta ya elimu, ambapo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kitashirikiana na Chuo cha Triumphant cha Namibia kufundisha lugha ya Kiswali kama nia ya kukuza uhusiano, urafiki na mshikamano kijamii.