Na Lucy Lyatuu
DAR ES SALAAM: KUELEKEA uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imejipanga kuelimisha wananchi kujua madhara ya rushwa na kuhamasiaha kushirikiana na taasisi hiyo kutokomeza vitendo hivyo.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU, wilaya ya Kinondoni, Elizabeth Mokiwa amesema hayo leo Dar es Salaam na kuongeza kuwa Taasisi hiyo itaendelea kupokea malalamiko yote yanayohusu rushwa na kuyafanyia kazi kwa uharaka ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo wakati wote.
Amesema rushwa katika uchaguzi husababisha kuchaguliwa kwa viongozi wasio waadilifu watakaotumia muda wao mwingi wa uongozi kurejesha fedha zao na siyo kuleta maendeleo kwa wananchi.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo na kuwasihi wenye taarifa zozote za rushwa kuwasiliana nao bure kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi kwa namba ya dharura 113 nakufuata maelekezo.
Kuhusu mikakati ya mwaka 2024 hadi 2025, TAKUKURU inatekeleza program ya Takukuru Rafiki kwa kufikia wananchi kwenye kata 20 na kupokea kero 61 na kuzitatua kero hizo kwa uharaka ili zisiwaathiri wananchi.
Amesema mirdi ya maendeleo 26 yenye thamani y ash bilioni 80.2 imefuatiliwa utekelezaji wake na kubainika kuwa na mapungufu machache ambayo wahusika wameshauriwa kuyarekebisha ili miradi ikaimilike kwa wakati na kwa thamani halisi.