Na Lucy Lyatuu,Dodoma
MAMLAKA ya Kudhibiti Na Kupambana Na Dawa Za Kulevya (DCEA) imesema iko kwenye mchakato wa kutunga sheria ya kudhibiti kiburudisho aina ya shisha kutokana na kubainika kuwekwa dawa za kulevya.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema hayo mbele ya Waziri wa wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu Na Wenye Ulemavu Profesa Palamagamba Kabudi wakati akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasilisha taarifa ya hali ya dawa za kulevya mwaka 2025.
Amesema shish imekuwa ikitumika vibaya kwa kuweka dawa za kulevya ambapo mchakazo huo utawezesha kuwa namsheria ya kuzuia kiburudisho hicho.

Kuhusu kilimo cha bangi nchini amesema mkoa wa Morogoro unaongoza kwa kilimo cha mmea huo ikifuatiwa na Mkoa wa Mara na Tabora.
Katika ripoti hiyo amebainisha kuwa kiasi cha bangi tani 1,757.56 ilikamatwa kwa mwaka 2023, huku mwaka 2024 ta I zilizokamatwa ni 2,303.20 na kwa mwaka jana ikiwa nimtani 1,014.
Amesema kuhusu idadi ya watuhumiwa wa bangi kwa mwaka 2024 ni watu 7981 huku mwaka jana wakiwa 7715, idadi ambayomimepungua kutokana na kuimarika kwa jitihada za utoaji elimu kwa jamii kuhusu tatizo lamdawa za kulevya.
Amesema bangi iliendelea kukamatwa kwa wingi na hata hivyo kiasi kilichokamatwa kilipungua kwa asilimia 55.97 ikilinganishwa na mwaka 2024.
Amesema upungufu huo unatokana na uteketezaji wa mashamba ya bangi uliofanyika mwaka 2024,kuimarika kwa udhibiti ikiwemo utoaji elimu kwa jamii inayojihusisha na kilimo cha bangi kuhusu madhara ya kilimo cha zao hilo.

