Na Lucy Lyatuu, Dodoma
SERIKALI imeainisha mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya bahari ikiwemo kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam kutoka tani milioni 16.27 mwaka wa fedha 2020/21 hadi kufikia tani milioni 27.76 mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 70.62.
Aidha imesema Kuongezeka kwa wastani wa shehena ya makasha yanayohudumiwa kwa mwezi kutoka makasha TEUs 61,000 hadi TEUs 102,000, sawa na ongezeko la asilimia 67.21.
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema hayo wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo Bungeni kwa mwaka 202627 na kuongeza mafanikio mengine ni Kupungua kwa gharama za uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kutoka Sh bilioni 652.83 mwaka 2023/24 hadi Sh bilioni 308.95 mwaka 2024/25.

Amesema mafanikio mengine ni Kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya TPA yatokanayo na ada za huduma za kibandari kutoka Sh bilioni 896.95 mwaka 2020/21 hadi kufikia Sh trilioni 1.30 mwaka 2024/25 na Kupungua kwa muda wa kuhudumia meli za makasha gatini kutoka wastani wa siku 10 hadi siku 3.
Profesa Mbarawa amesema mafanikio mengine ni Kupungua kwa muda wa meli kusubiri nangani kutoka wastani wa siku 46 hadi wastani wa siku saba kwa meli za mizigo mchanganyiko na kichele, Hatua za Serikali Kukabiliana na Ongezeko la Shehena katika Bandari ya Dar es Salaam.
Amesema Kutokana na kuongezeka kwa ufanisi wa Bandari ya
Dar es Salaam kumeimarika kwa imani va Watumniaji wa bandari hio, Kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya TPA yatokanayo na ada za huduma za kibandari kutoka Sh bilioni 896.95 mwaka 2020/21 hadi kufikia Sh trilioni 1.30 mwaka 2024/25.
Amesema Kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya TPA yatokanayo na ada za huduma za kibandari kutoka Sh bilioni 896.95 mwaka 2020/21 hadi kufikia Sh trilioni 1.30 mwaka 2024/25 na Kupungua kwa muda wa kuhudumia meli za makasha gatini kutoka wastani wa siku 10 hadi siku tatu.
Ameongeza mafa ikio mengine ni Kupungua kwa muda wa meli kusubiri nangani kutoka wastani wa siku 46 hadi wastani wa siku 7 kwa meli za mizigo mchanganyiko na kichele, Hatua za Serikali Kukabiliana na Ongezeko la Shehena katika Bandari ya Dar es Salaam
Amesema , Kutokana na kuongezeka kwa ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuimarika kwa imani ya watumiaji wa bandari hiyo ndani na nje ya nchi, kumekuwepo na ongezeko kubwa la shehena ya mizigo inayohudumiwa bandarini. li kuhakikisha bandari inaendelea kutoa huduma kwa ufanisi, ushindani na viwango vinavyokidhi mahitaji yanayoongezeka.

