MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yachukua Hatua Madhubuti Kukuza Ajira kwa Wahitimu wa Vyuo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yachukua Hatua Madhubuti Kukuza Ajira kwa Wahitimu wa Vyuo
Habari

Serikali Yachukua Hatua Madhubuti Kukuza Ajira kwa Wahitimu wa Vyuo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: SERIKALI imeendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha wahitimu wa vyuo wanapata fursa za ajira kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati, uendelezaji wa viwanda vidogo na vya kati pamoja na programu za ubunifu nchini.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, Rahma Kisuo, leo Januari 30, 2026, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Dkt. Regina Malima aliyehoji mikakati ya Serikali katika kuongeza ajira kwa wahitimu wa vyuo.
Kisuo amesema kupitia miradi ya kimkakati, Serikali imefanikiwa kuzalisha ajira nyingi ikiwemo zaidi ya ajira 35,000 zilizotokana na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), pamoja na zaidi ya ajira 10,000 kutoka katika mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).
Habari Picha 10982
Ameongeza kuwa miradi mingine iliyochangia upatikanaji wa ajira ni pamoja na ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Mwalimu Julius Nyerere uliotoa zaidi ya ajira 10,000 na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato jijini Dodoma uliotoa zaidi ya ajira 1,500,
Pia ujenzi wa Daraja la JPM (Kigongo–Busisi) uliotoa zaidi ya ajira 1,500, pamoja na upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam uliotoa zaidi ya ajira 3,000.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri amesema Serikali pia imetoa mafunzo ya uzoefu wa kazi kwa wahitimu 29,902 wa ngazi mbalimbali za elimu, sambamba na kutoa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi 19,075 katika sekta za hoteli, madini, usafirishaji, kilimo na usindikaji wa mazao ya kilimo kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali imeandaa Mwongozo wa Taifa wa Mafunzo kwa Vitendo kwa Wahitimu unaolenga kuweka utaratibu wa utoaji wa mafunzo ya uzoefu wa kazi kwa wahitimu.
Mwongozo huo unatumika kwa waajiri wote katika sekta ya umma na binafsi ili kuhakikisha wahitimu wanapata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira.

You Might Also Like

Mvua, Upepo Yaharibu Shule Lindi, Serikali Yatoa Milioni 96

Waziri Mkuu Majaliwa ndani ya SGR

Watanzania Acheni Kuchanganya Mazao -Jafo

Thamani ya Fedha Ionekane Kwenye Utekelezaji wa Miradi-Nyamoga

Matumizi Holela Ya Vilevi Hatari Kwa Watumiaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Jafo Ahoji Fedha Za Ujenzi Barabara Ya Mzenga – Kisarawe
Next Article Mbunge Mgalu Auliza Hatima ya Ujenzi wa Chuo cha VETA Bagamoyo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?