MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ridhiwani  Azindua Hafla ya Kuupandisha Mwenge, Mlima Kilimanjaro
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ridhiwani  Azindua Hafla ya Kuupandisha Mwenge, Mlima Kilimanjaro
Habari

Ridhiwani  Azindua Hafla ya Kuupandisha Mwenge, Mlima Kilimanjaro

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

KILIMANJARO: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema Mwenge wa Uhuru umepelekwa juu ya Mlima Kilimanjaro baada ya kuhitimisha mbio kwa siku 195.

Ridhiwani amesema hayo ikiwa ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kwamba mwaka huu 2024, mwenge huo baada ya kuhitimisha mbio zake upelekwe katika mlima huo.

Amesema kitendo cha kupeleka mwenge huo juu ya mlima Kilimanjaro kinaitangazia dunia kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni imara, na kwamba Tanzania itaendelea kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Ridhiwani amesema hayo katika hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakati wa hafla ya kupokea kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambacho kimepewa jukumu la kupeleka Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania kilele cha mlima Kilimanjaro.

Pia Ridhiwani amehamasisha vijana kuendelea kuenzi falsafa za mwenge wa uhuru ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961.

Awali akizungumza, Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana amesema kupandishwa mwenge wa uhuru Mlima Kilimanjaro mwaka huu 2024 kunaleta hamasa ya uzalendo kwa wananchi hususan wakati huu ambao Tanzania inaadhimisha miaka 60 ya uhuru na mafanikio ya Taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amemshukuru Rais Samia kwa kuridhia mwenge wa uhuru kupandishwa kwa mara nyingine katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Kiongozi wa kikosi hicho Maalum, Luteni Kanali Khalid amemhakikishia Waziri Ridhiwani kuwa kikosi hicho kinaufikisha, kinaulinda na kuutunza Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania hadi katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

You Might Also Like

Kingalame Asisitiza Umuhimu wa Wachimbaji Kuuza Dhahabu Serikalini

Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Wanaotumika Vibaya Waonywe

Wenye Ulemavu Wa Ngozi Wakumbukwa Kupitia FDH, Wapewa Msaada Wa Milioni 20

Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Petroli Afrika

TRC, Wananchi Burundi Wakutana Utekelezaji Mradi wa SGR

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Hakuna Vituo Bandia vya Kuandikisha Wapigakura:Mchengerwa
Next Article Silaa: Akili Mnemba, Roboti kuongeza ufanisi,ubunifu 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Diwani Kata Ya Majengo Awasihi Wananchi Kufanya Kazi Kwa Bidii
Habari February 16, 2026
Tanzania Yalenga Kufikia Asilimia 51 Ya Ushiriki Wa Wanawake Katika Sayansi
Habari February 14, 2026
Makamu wa Rais Asisitiza Ubunifu, Uwekezaji Soko La Hisa La Dar es Salaam
Habari February 13, 2026
JAB Yasisitiza Ithibati Kama Njia ya Kuimarisha Ubora na Uaminifu wa Habari
Habari February 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?