Na Mwandishi Wetu
RAIS Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mkoani Kilimanjaro.
Samia anaelekea mkoani Arusha ambapo atakuwa mgeni rqsmi katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kitakachofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kesho tAgosti 28, 2024.
Rais Samia ametokea nchini Kenya ambapo alihudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga, anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Agosti 27, 2024