MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Rais Samia Atoa Bil. Nne Ujenzi Kiwanda Cha Kuzalisha  Nishati Mbadala  
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Rais Samia Atoa Bil. Nne Ujenzi Kiwanda Cha Kuzalisha  Nishati Mbadala  
Habari

Rais Samia Atoa Bil. Nne Ujenzi Kiwanda Cha Kuzalisha  Nishati Mbadala  

Author
By Author
Share
5 Min Read

 Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) wamesaini mkataba wenye lengo la kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha nishati mbadala mkoani Geita ambapo mkataba huo una thamani ya sh bilioni 4.5.

Katika hafla iliyofanyika katika Ofisi ndogo ya REA, Jijini Dar es Salaam, REA itatoa jumla ya sh bilioni tatu na STAMICO itatoa sh bilioni 1.5.

Kwa mchanganuo huo, REA itagharamia ununuzi wa mtambo wakati STAMICO italipia upatikanaji wa kiwanja, ujenzi wa jengo la kiwanda na gharama za ufungaji wa mitambo.

Mkataba huo umesainiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa REA Hassan Saidy, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse.

Mkataba huo utaifanya STAMICO kuwa na viwanda vikubwa vitano vya kuzalisha mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes; viwanda vingine ambavyo vinaendelea na uzalishaji wa mkaa mbadala vipo wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Kiwira mkoani Songwe, na viwanda vingine viwili vipo mkoani Dodoma na Tabora ambapo vipo kwenye hatua za mwisho za ukamilishwaji kabla kuanza uzalishaji.

Akizungumza  katika hafla hiyo,  Hassan Saidy, amesema kuwa Wakala umepewa jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia unafikia asilimia 80 kwa Watanzania wote ifikapo mwaka 2034.

“Katika kufanikisha lengo hilo, Wakala unatekeleza Miradi mbalimbali ikiwemo uwezeshaji katika kuongeza uzalishaji na usambazaji ili kuongeza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa Watu wa vijijini.”

“Utiaji wa saini wa Mkataba huo kati ya REA na STAMICO ni moja wapo ya utekelezaji wa maagizo ya Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Wakala ili kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa kuona namna ya kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nishati safi kwa Wananchi ili waondokane na matumizi ya nishati zisizo safi na salama”. Amesema Hassan.

“Ni matumaini yetu kuwa Mkataba huu utaende kuongeza kasi ya upatikaji wa mkaa mbadala na kwa bei nafuu ikiwa ni mojawapo ya lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia. Tunatambua kuwa utunzaji wa mtambo huu ni muhimu sana ili huduma iliyokusudiwa iendelee kutolewa kwa wakati bila kuathili uchumi wa Wananchi, afya na pamoja na mazingira kwa ujumla”. Ameeleza Hassan .

Saidy ameongeza kuwa Wakala unaendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kuhakikisha Mkakati wa Nishati safi ya kupikia unatimiza malengo yaliyowekwa, ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji na usambazaji wa mkaa mbadala.

Wakala unaendelea kutekeleza Miradi mbalimbali ikiwemo usambazaji wa majiko banifu, usambazaji wa majiko ya umeme, usambazaji wa mitungi ya gesi ya kupikia majumbani (LPG ya kilo 6 na 15); usambazaji wa gesi asilia katika mkoa wa Lindi na Pwani pamoja na ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia katika Taasisi za Umma.

Kwa upande wake, Dkt.  Mwasse, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO ameishukuru Serikali kupitia REA kwa mchango huu ambao utasaidia Shirika hilo  kutimiza ndoto yake ya kuhakikisha wananchi wote wanaachana na nishati isiyo safi na salama ya kupikia ifikapo mwaka 2034 na hivyo kuunga mkono juhudi za Serikali za kutunza mazingira.

“Hii ajenda ya matumizi ya nishati safi ambayo kinara wake ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inalenga kumkomboa Mwanamke ili aachane na nishati isiyo safi na salama. STAMICO tumejipanga kutekeleza maono haya ya Kiongozi wetu”, amesema Dkt. Mwasse.

Ameongeza kuwa nishati ya Rafiki Briquettes kwa sasa inatumiwa na Jeshi la Magereza ambapo Magereza yote 129 nchini kote yanatumia nishati hii kama aina mojawapo ya nishati ya kupikia, vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Taasisi nyingine ni pamoja na vyuo mbalimbali vya mafunzo, shule za msingi na sekondari, hoteli, migahawa, na sehemu wanazochoma nyama na chipsi.

Dkt. Mwasse amesisitiza kuwa STAMICO itaendelea kutunza mitambo hiyo ili iendelee kutoa huduma kwa Wananchi.

 

 

 

You Might Also Like

‘Jichunge’ Programu Ya Simu Yenye Mafanikio Katika Kuboresha Matumizi Ya Dawa Kinga Dhidi Ya VVU

Biteko Agongea Msumari Elimu Ya Ufundi Stadi

COSTECH Yasaini Mkataba Ujenzi Jengo La Sayansi, Teknolojia, Ubunifu

Nyamhokya: Mei Mosi Ni Singida Mwaka Huu 2025

Elimu Ya Fedha Yafika Makanya Same

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ziara ya Kwanza ya Kiongozi wa Juu wa Tanzania Nchini Belarus Yafungua Ukurasa Mpya wa Ushirikiano
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ziara ya Kwanza ya Kiongozi wa Juu wa Tanzania Nchini Belarus Yafungua Ukurasa Mpya wa Ushirikiano
Habari July 22, 2025
Mapinduzi ya Elimu Geita: Wasichana Wamerudi Shule kwa Kasi
Habari July 21, 2025
Vijana Ni Chachu Ya Maendeleo Endelevu Wakiwezeshwa-Kikwete
Habari July 21, 2025
Ikomba: Aliishi Na Watoto Wiki Sita Akiwafundisha Kabla Ya Mtihani WaTaifa
Habari July 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?