Shirila La Posta Tanzania limekuja na ubunifu mpya Wa mabasi madogo ya kitalii ambayo yanatumika Kusafirisha viongozi na wananchi kutoka kwenye eneo la mapokezi ya maonesho ya biashara ya kimaraifa maarufu kama sabasaba Ili kuzunguka eneo lote kwa watakaohitaji.
Gharama za Kupata usafiri huo ni sh 2000 kwa mtu mzima na kwa mtoto sh 1000 ambapo wananchi wamekuwa wakitumia fursa hiyo kuzunguka manenobalimbali ya maonesho.
Kuhusu Maonesho hayo Shirika hilo Posta Masta Mkuu MKUU Macrice Mbodo amesema mbali na huduma ya Usafiri pia Shirika limejipanga kusafirisha vifurushi na mizigo kutoka ofisini kwako au nyumbani kwa mteja mpaka kwenye banda la mhusika katika viwanja vya sabasaba na kurejesha ofisini kwa mhusika au nyumbani baada ya kukamilika kwa maonyesho ya sabasaba.
Aidha katika maonesho hayo pia Shirika Shirika la Posta Tanzania linatoa huduma ya kusafirisha vifurushi na mizigo itakayonunuliwa na wateja kwenye maonesho ya sabasaba kutoka kwenye banda itakaponunuliwa bidhaa hizo na kuzifikisha nyumbani kwa mteja.
Vilevile Shirika linafanya clearing and forwarding kwa wafanyabiashara washiriki wa maonesho
kutoka nje ya mipaka yaTanzania.
“Kwa uhuru wa watakaokuwa na mabanda kwenye maonyesho ya sabasaba, tutaweka
bidhaa zao kwenye duka letu mtandao ili kuwafanya wananchi na wageni kutoka nchi
zingine duniani kushiriki maonyesho haya ya sabasaba kwa kununua bidhaa yoyote
itakayosajiliwa kwenye duka letu mtandao,
na sisi kumsafirishia bidhaa hiyo na
kumfikishia popote pasipo yeye kulazimika
kuja kwenye maonyesho,” amesema.
Amesema Lengo ni kuwapa fursa ya pamoja wananchi waliyoko nje ya mkoa wa Dar es salaam na nje ya Tanzania kushiriki maonyesho hayo ya sabasaba kidijitali sawasawa na fursa waliyonayo wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.