Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: VIKOSI vyote vya Jeshi la Polisi Kanda Maalun ya Dar es Salaam vimejipanga kuimarisha ulinzi kwenye nyumba za ibada ili kuwawezesha wananchi kushiriki ibada zilizoandaliwa msimu huu wa sikukuu za krismas 2024 na mwaka mpya 2025.
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari ofisiini kwake Leo Disemba 21, 2024 ikiwa ni maandalizi ya kuelekea sherehe za mwisho wa mwaka Krismas na mwaka mpya.
Muliro ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na aina ya
vitendo ambavyo vinaweza kusababisha kutendeka kwa makosa ikiwemo kuendesha vyombo vya moto bila kuzingatia sheria za usalama barabarani.

“Kutumia vilevi wakiwa wanaendesha vyombo
vya moto , na mambo mengine yaliyo kinyume na sheria. Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali na za haraka za kisheria kwa wote watakaobainika kutenda makosa hayo.
vya moto , na mambo mengine yaliyo kinyume na sheria. Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali na za haraka za kisheria kwa wote watakaobainika kutenda makosa hayo.
“Jeshi la Polisi linawaonya na kutao tahadhari watu wenye tabia ya kupiga baruti au fataki bila vibali vya kisheria na maeneo ambayo hayaruhusiwi na sheria, Polisi hawatasita kuchuka hatua kwa mtu yote atakayekiuka sheria za nchi kwa kisingizio cha kufanya mambo ya ovyo chini ya mwavuli wa Krismasi na mwaka mpya,” amesema.