Na Lucy Lyatuu,Dodoma
OFISI ya Taifa Ya Takwimu inatarajia kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo ya huduma za kifedha kwa wafanyabiashara 815 wakiwemo Wakala wanaotoa huduma hizo.
Lengo la utafiti huo ni Serikali kupata takwimu zitakazotumika kupima maendeleo ya utekelezaji wa mikakati wa Taifa wa ujumuishaji wa kifedha.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt Amina Msengwa amesema hayo jijini hapa wakati akizungumza kuhusu kuanza kwa tafiti mbalimbali zenye lengo la kukusamya taarifa muhimu kuhusu shughuli za biashara katika sekta rasmi na zisizo rasmi.
Amezitaja tafiti zitakazofanywa na Ofisi hiyo kuwa ni utafiti wa kina wa shughuli za kibiashara,utafiti wa sekta isiyo rasmi,utafiti wa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo sana,wadogo na wa katika na utafiti wa uzalishaji viwandani.
Amesema katika tafiti hizo unawezesha kupata taarifa za ajira, uzalishaji viwandani ,uwekezaji na mazingira ya biashara ambayo yatabainisha mwenendo wa ukuaji wa biashara na viwanda nchini.
Amesema taarifa zitakazopatika a zitaiaaidia Serikali na wadau wa sekta binadsi,mashirika yasiyonya kiserikali na watafiti kubuni programu mbalimbali za kubotesha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini na kuhuisha takwimu za thamani ya Pato ghafi.
Kuhusu utafiti kuhusu huduma za biashara amesema zitatumika kupima maendeleo ya utekelezaji wa mikakati wa Taifa wa ujumuishaji wa kifedha awamu ya tati pamoja na mpango Mkuu wa maendeleo ya sekta ya fedha hususani katika kutoa ushahidi wa kitakwimu kuhusu upatikanaji wa mikopo,akiba na huduma za fedha za kidigitali Kwa biashara mdogo sana na za kati.
Amesema matokeo ya utafiti huo utasaidia katika kuimarisha juhudi za kuendeleza sekta ya fedha nchini na kubotesha utoaji wa bidhaa na huduma za fedha zinazokidhi mahitaji ya wafanyabiashara.
Amesema tafiti hizo zitafanyika nchi nzima kwenye maneno ambayo yamechaguliwa ambayo yanafikia 1518 ikiwemo maneno 703 Kwa ajili ya utafiti wa sekta isiyo rasmi na maneno 815 Kwa ajili ya utafiti wa huduma za fedha.
Aidha amesema utafiti wa kina wa shughuli za biashara utahusisha taasisi na biashara 8624 na utafiti wa uzalishaji viwandani ukihusisha maneno 4245.
Dkt Msengwa amesema katika utafiti huo watategemea kuwa na wadadisi 713 na wasimamizi 69 ambayo jukumu lao ni kuhakikisha taarifa zinazokusanywa zina ubora wa Hali ya juu.
“Wakati wa utekelezaji wa tafiti hizo wadadisi watajitambulisha kwenye kaya na viongozi wa Serikali za mitaa na Kwa upande wa taasisi na viwanda wadadisi watakuwa na barua za utambulisho kutoka kwenye uongozi wa mkoa au halmashauri.

