MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: NIT yawapika vijana
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > NIT yawapika vijana
Habari

NIT yawapika vijana

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
WANAFUNZI kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wamefika katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wafanyabiashara, wakiwa na teknolojia za kilimo na ufugaji.
Teknolojia hizo zinamrahisishia
 mkulima kutumia nyenzo rahisi za uchakataji mazao.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Chuo hicho,Mwalimu aliyeambatana na wanafunzi waliotengeneza bunifu hizo Kelvin Odhiambo amesema, wamekwenda na wanafunzi wao ili kuonesha bunifu wanazotengeneza kwa sababu zinawahusu na zinaweza kuwasaidia wakulima.
Amesema, wanafunzi hao wametengeneza mashine za kuchakata vyakula mbalimbali , mashine ya kusambaza mbolea na mashine ya kufugia vifaranga vikiwa bado vidogo.
Amewaasa vijana na wananchi kwa ujumla wenye sifa kujiunga na chuo hicho ili waweze kupata ujuzi wa bunifu mbalinbali.
“Tayari NIT imefungua dirisha la usaili kwa ngazi ya stashahada na shahada ,waliomaliza kidato cha nne na cha sita wanakaribishwa kujiunga na chuo hicho.”amesema Mhandisi Odhiambo
Mwanafunzi wa chuo hicho George Valentine amesema ametengeneza mashine ya kufugia vifaranga vya kuku mara baada ya kutotolewa ili viweze kuwa salama dhidi ya ndege na wanyama kama paka,panya na mbwa.
“Mashine hii ni nzuri kwa kufugia vifaranga,baada ya kuzaliwa na kupewa chanjo,vifaranga vinatunzwa katika mashine hii na vinakuwa salama dhidi ya panya,ndege na wanyama wanaokula vifaranga lakini pia vinapata joto linalohitajika pamoja na chakula na maji kwa wakati unaohitajika.”amesema George
Amesema mashine hiyo kutoa taarifa pale chakula na maji vinapopungua.
Naye Omary Athumani mwanafunzi wa chuo hicho amesema amekuja na mashine ya kuchanganya chakula cha mifugo ambayo kukoboa na kusaga kwa wakati mmoja na mashine ya kutengeneza siagi na kutoa mafuta kwa wakati mmoja.
“Mashine hii ina uwezo wa kutengeneza bidhaa husika kwa kilo 100 kwa saa moja.”
Amesema,ametengeneza mashine hizo ili kumsaidia mkulima dhidi ya mazingira magumu ambayo anapitia kwani kupitia mashine hiyo mkulima anaweza kuchakata mazao yake na kuuza mazao yaliyochaktwa na kupata faida badala ya kuuza mazao ghafi.

You Might Also Like

Washauriwa Kutumia Mbegu Zinazokabiliana Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi

Rais Mwinyi adhamiria kusimamia ubora wa bidhaa

MAIPAC Yagawa Makoti Ya Usalama Kwa Wanahabari Kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Mafunzo ya Ufundi Sasa Kupatikana Popote Kupitia Programu ya VSOMO”

TEA Kukarabati Jengo La Bodi Ya Maktaba Kwa Milioni 300

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Jisajilini mapema mpate mbolea ya ruzuku
Next Article Shemdoe apongeza
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?