Lucy Ngowi
DODOMA: WANACHAMA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF),, hivi sasa wanaweza kupata huduma za matibabu kwa kutumia namba ya Kitambulisho cha Uraia (NIDA).
Kaimu Meneja kutoka Kitengo cha Mawasiliano NHIF, Grace Michael amesema hayo katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea Jijini Dodoma.
Amesema mfuko huo umeendelea kurahisisha huduma zake hususan ya utambuzi wa mwanachama anapokuwa katika vituo vya kutolea huduma kwa kutumia namba hiyo ya NIDA.
“Kwa sasa mwanachama wa NHIF anaweza akatambuliwa kituoni kwa kutumia namba ya NIDA. Hii itaondoa changamoto kwa wale waliokuwa wanasahau vitambulisho nyumbani.
” Mwanachama hatalazimika kutembea na kadi hata wale wanaopoteza hizo kadi nao wanaenda kuondoa usumbufu.
“Wanachama watumie fursa hii kuhuhisha taarifa zao za NIDA. Walioko hapa watenbelee banda letu,” amesema.
Ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa ya kujiunga na mfuko huo kwa sababu ugonjwa unampata mtu bila taarifa.