Na Lucy Ngowi
MWANACHAMA wa Chama Cha Watumishi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), Irene Mwakabanga amekutwa hana hatia katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili.
Irene alishtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi na. nane ya mwaka 2023 ambayo ilianza kusikilizwa Novemba 28, mwaka jana 2023.
Amesema ilipofika jana Oktoba 31, kesi hiyo ilihitimishwa kwa kupata ushindi kwa kuwa upande wa serikali kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha.
Kutokana na ushindi huo, ameshukuru chama cha TALGWU kwa kumpatia wakili aliyesimamia kesi yake hadi kukutwa hana hatia.
Irene ametoa shukrani hizo muda mfupi baada ya kupata ushindi huo.
Alifanya kazi halmashauri ya Ngara Bukoba, mwaka 2018 hadi mwaka jana, na sasa ni Ofisa Biashara Halmashauri ya Mafinga mkoani Iringa.