MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Munde Aahidi Kuboresha Miundombinu, Uchumi Wa Liwale
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Munde Aahidi Kuboresha Miundombinu, Uchumi Wa Liwale
Habari

Munde Aahidi Kuboresha Miundombinu, Uchumi Wa Liwale

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Liwale mkoani Lindi, Mshamu Munde, ameapishwa rasmi leo, Novemba 12, 2025, na kuahidi kushirikiana na wananchi kuharakisha maendeleo ya jimbo hilo.
Ahadi hiyo ameitoa muda mfupi baada ya kuapishwa katika viwanja vya Bunge alipozungumza na waandishi wa habari.
Munde amesema anaingia bungeni akiwa na dhamira ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Liwale, hususan tatizo la miundombinu ya barabara, kilimo na huduma za kijamii.
 “Changamoto kubwa kwa muda mrefu imekuwa ni barabara ya Liwale–Nangurukuru, ambayo inaunganisha barabara kuu ya Lindi–Dar es Salaam. Tatizo hili sasa linapatiwa ufumbuzi kupitia Ilani ya CCM,” amesema.
Habari Picha 10274
Kwa mujibu wa Ilani hiyo, barabara ya Liwale–Nangurukuru itajengwa kwa kiwango cha changarawe chenye madaraja na mitaro bora, ili iweze kupitika kwa mwaka mzima.
“Barabara hii ikikamilika itakuwa mkombozi wa kiuchumi. Wananchi hawatalazimika tena kupanga safari kutokana na mvua, na usafirishaji wa mazao utaimarika,” amesema Munde.
Aidha, amesema barabara ya Liwale–Nachingwea itajengwa kwa kiwango cha lami, hatua itakayowezesha wananchi kupata mtandao mzuri wa usafiri kuelekea Lindi na Dar es Salaam, hivyo kuchochea biashara na uwekezaji.
Akizungumzia sekta ya kilimo, Munde amesema wakati huu Liwale inategemea zaidi zao la korosho, lakini amepanga kuhamasisha uzalishaji wa ufuta, alizeti na chikichi ili kuongeza vyanzo vya mapato.
“Tukifanikiwa kuwa na mazao manne ya uhakika, kipato cha wananchi kitaongezeka mara nne kwa mwaka,” amesema.
Mbunge huyo amehitimisha kwa kusema ataendelea kushirikiana na serikali kuboresha huduma za elimu, afya na maji, akisisitiza kwamba maendeleo ya Liwale yatachochewa zaidi kwa ushirikiano wa karibu kati ya wananchi na viongozi wao.

You Might Also Like

CHAUMMA YAAPA KUJENGA BUNGE LA WABUNGE WA HOJA, SI MACHAWA

Tanzania Kushirikiana na Finland Uboreshaji Mbegu za Miti

Mwalim: Mchagueni Mwalimu Wangu Wa Siasa Shibuda

TEA Kukarabati Jengo La Bodi Ya Maktaba Kwa Milioni 300

SOKO LA MADINI LA 43 LA ZINDULIWA TUNDURU RUVUMA.

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kagae: Waziri Mkuu Ajaye Atamsaidia Rais Samia Kuongeza Kasi ya Maendeleo
Next Article Mbunge Ulanga Aweka Mikakati Kuufungua Mkoa wa Morogoro Kimaendeleo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?