Na Danson Kaijage
DODOMA: BOHARI kuu ya dawa (MSD) imesema kipindi cha Julai mwaka jana 2024 mpaka sasa imeokoa kiasi cha Sh. Milioni 15.8 kutokana na kubana matumizi yasiyokuwa ya lazima.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Bohari ya Dawa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 19, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

Pamoja kuokoa fedha ambazo zilikuwa katika mfumo wa matumizi yasiyokuwa ya lazima pia mfumo wa matumizi ya TEHAMA umesaidia kudhibiti upoteaji wa dawa na vifaa tiba au udanganyifu ambao ulikuwa ukijitokeza.
Amesema.kuwa kwa kipindi cha miaka minne MSD imefanikisha kupeleka dawa na vifaa tiba katika vituo vyote vya afya nchini na kwa wakati jambo ambalo halijawahi kutokea kwa miaka ya nyuma.
Ameongeza kuwa kwa sasa nchini kuna vifaa vya kisasa vya kuchuja damu na kwa kuwa na vifaa hivyo imepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha ambazo zingetumia kwa ajili ya matibabu ya nchi.