Na Sixmund Begashe – Iringa
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba, amepongeza kazi nzuri na kasi ya ujenzi wa Kituo cha Utafiti cha Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) .
Kituo hicho kinajengwa kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).

Wakulyamba ametoa pongezi hizo alipotembelea eneo la Kihesa Kilolo Iringa, kunapotekelezwa Mradi wa REGROW kwa lengo la kujionea namna hatua za utekelezaji wa mradi huo.
Akitembela Kituo cha taarifa kwa wageni chini ya Bodi ya Utalii Tanzania, Wakulyamba hakuridhishwa na kasi ya Mkandarasi wa jengo hilo, na kumtaka ajitafakari kwa kuwa hadi sasa yupo nyuma ya malengo yaliyowekwa.
Naye Mhandisi Mkazi na Meneja wa Mradi, Wilfred Saitoria, ameelezea kuwa utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo ni kuwa jengo la TAWIRI limefikia asilimia 67 zaidi ya lengo kuwa ilikuwa lifikie asilimia 46 na linajengwa na jengo la TTB limefikia asilimia 28 wakati ujenzi ukitakiwa uwe umefika asilimia 64 .