Na Lucy Ngowi
RAIS Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu David Cleopa Msuya kilichotokea leo Mei saba, 2025.
Aidha amesema taarifa zaidi ya Mipango kamili ya msiba itaendelea kutolewa na Serikali.
Samia amesema Msuya amefariki katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Kutokana na msiba huo, Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo Mei saba hadi 13, 2025.
Rais Samia anawapa pole ndugu, jamaa na watanzania wote kwa msiba huu.