Na Lucy Lyatuu,Tanga
SHIRIKA La Kilimo Na Chakula Duniani (FAO) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) wanatekeleza mfumo wa kuongeza masoko kwa wauzaji,wachakataji na wavuvi wa samaki ujulikanao Tanfish ambapo mpaka sasa umewafikia watumiaji 700.
Mhandisi wa Mifumo Ya Kidigitali kutoka UDSM, Shabo Andrew amesema hayo wakati akizungumza katika siku ya chakula duniani katika maadhimisho yanayofanyika mkoani Tanga kwenye viwanja vya Usagara.
Amesema hadi kufikia Juni 2026 mahitaji ya tani sita hadi saba yamefikiwa ambapo uhitaji wa bidhaa hiyo ni mkubwa na hata wanaohitaji kuutumia mfumo kwa kila mkoa.
Amesema mfumo ulianzia katika Kanda ya ziwa Tanganyika na Viktoria ambapo uhitaji ulikuwa mkubwa lakini pia kwa wavuvi wa baharinya Hindi wakiomba kutumia mfumo huo ambao ulitengenezwa na UDSM huku FAO wakiwezesha kukusanya data,kutoa mafunzo na hata tafiti mbalimbali kuhusu mfumo huo.
Amesema mfumo unapatikana kwa njia ya kidigitali kwenye Play store na appStore ambapo mtumiaji anaupakua na kuanza kuweka bidhaa zake ambazo zitaonekana nchi nzima hata nje ya nchi na wateja kupatikana.
“Kupitia mfumo wa Tanfish mteja anaweza kuona bidhaa za samaki na akiweka oda, Tanfish wanasimamia usafirishaji kuhakikisha bidhaa inamfikia mhusika ikiwa salama popote alipo,” amesema na kuonageza kuwa kila.mkoa wauzaji wanataka kuutumia mfumo.
Amesema kanda ya kati imekuwa ndio watumiaji wakubwa lakini pia kuna uhitaji nje ya nchi na changamoto kubwa ikiwa ni upatikanaji wa leseni zinazoruhusu.
Amesema kupitia mfumo huo ni fursa kwa makundi mbalimbali kushiriki na kwamba wauzaji ni wa ndani ya nchi na wapo wanunuaji nje ya nchi.
Amesema kupitia siku ya chakula ni fursa kwa wananchinwa Tanga kuutumia mfumo kuagiza na kuuza hata kama ni jumla au rejareja ili kukuza kipato na kuimarisha lishe.
Maoni 0
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!