Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: SERIKALI imeshauriwa kuangalia namna ya kuwepo kwa miongozo kwa ajili ya wagunduzi wa teknolojia mbalimbali.
Ushauri huo umetolewa na Mbunifu Ernest Maranya kutoka Taasisi ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini (VETA), wakati wa kongamano la Kisayansi linalofanyika jijini Das Salaam lililoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),.
Amesema ili kuhakikisha wagunduzi na wabunifu wanaeleweka kisheria kuna kila sababu ya wadau wa elimu kuhakikisha inakuwa na muongozo kwa ajili ya wabunifu.
Kwa upande mwingine, Maranya amebuni kifaa kinachotoa elimu ya anga kwa kusema kuwa ipo haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuharakisha elimu ya anga kwa kutumia mfumo unaofanya kazi zaidi ambao utatumika shule zote.
Ameiomba serikali na wadau wa elimu nchini kumuunga mkono katika kufanikisha ubunifu anaoufanya.
Amesema pamoja na kugundua mfumo huo bado haujaanza kutumika mashuleni.