Na Mwandishi Wetu
PWANI:WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete pamoja na Mwenyekiti wa CCM, Mkoani hapa, Mwinshehe Mlao wakinadi wagombea wa chama hicho katika Kata ya Bwilingu.

Mbali na kunadi wagombea hao wameimarisha chama hicho kwa kuzindua mashina mapya manne ya wanachama wakereketwa katika kitongoji cha Bwilingu.
Ridhiwani amesema mapokezi ya wananchi yanaashiria ushindi wa chama hicho.


