MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata Waaswa kuwa wabunifu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata Waaswa kuwa wabunifu
Habari

Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata Waaswa kuwa wabunifu

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu Arusha

KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amewataka Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata kuwa wabunifu katika kusimamia uwajibikaji na kuongeza vyanzo vya miradi kutokana na fursa zilizopo kwenye maeneo yao.

Missaile ametoa kauli hiyo leo Agosti 08 , 2024 Jijini Arusha wakati akifungua mafunzo kwa Maofisa Tarafa na Watendaji wa Kata katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Amewataka Viongozi na Watendaji hao kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato ya Serikali na kuhimiza uwajibikaji wa watumishi.

“lakini mara nyingi tumekuwa hatuna ubunifu wa usimamizi na uwajibikiaji, tuna fursa nyingi za kiuchumi lakini hatuna ubunifu, hatusimamii, fursa za kijamii zinazopatikana kule hatuzielezei vizuri” alisema Missaile Musa.

Amesema uwepo kwa changamoto zinazotokana na kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji kazi wa kila siku kwa viongozi na watendaji hao katika ngazi ya msingi zitapata suluhu baada ya mafunzo hayo hususani masuala ya maadili, uzalendo na masuala ya kiutumishi.

Aidha, amewataka kuelewa majukumu yao kwa kina ili kuepuka muingiliano wa kimajukumu lakini pia kwa Maafisa Tarafa kufahamu masuala ya kisera na kuhimiza utekelezaji wake na Watendaji Kata kuandaa Mpango kazi wa Kata ili kuwa na agenda ya pamoja katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Naye Ibrahim Minja Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na ofisi yake kupitia Programu ya Uimarishaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Regions and Local Government Strengthening Programme-RLGSP), kwa kushirikiana na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na Chuo cha Utumishi wa Umma.

Amesema jumla ya washiriki 181 ambao ni Watendaji wa Kata 157 na Maafisa Tarafa 23 wanatarajiwa kupatiwa mafunzo hayo ili kwenda kuimarisha utendaji wao wa kazi kwenye maeneo yao.

Aidha, amesema katika awamu hii ya mwisho inahusisha mikoa nane ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma ambapo Maafisa Tarafa 203 na Watendaji wa Kata 1,377 watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo.

Kwa upande wake Edward Nguni Mtendaji wa Kata ya Naikanuka Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro amesema mafunzo hayo yatamwongezea weledi wa kazi na kuboresha ushirikiano na watumishi wa Sekta zote katika eneo lake yeye akiwa kiungo muhimu Pamoja na kuweza kutatua kero na migogoro ya wananchi kabla ya viongozi kufanya ziara katika eneo lake.

You Might Also Like

NEMC Kupambana Na Magugu Maji Ziwa Victoria

Biashara kidijitali inawezekana soko huru la Afrika

TDB Yaheshimisha Tasnia Ya Maziwa

Wakulima Wa Mahindi Mvomero Walia Na Viwavijeshi Vamizi, Watafiti SUA kupitia Mradi Wa AGRISPARK Kuokoa Jahazi

Wadau wa uchukuzi zingatieni maslahi ya wafanyakazi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Siri ya ushindi JKT hii hapa
Next Article Dkt. Bwana: Tunafanya utafiti wa mbegu kutatua changamoto za wakulima
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?