MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kumekucha Uzinduzi wa Washirika wa Tamasha, Tuzo Za Filamu Tanzania 2025
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kumekucha Uzinduzi wa Washirika wa Tamasha, Tuzo Za Filamu Tanzania 2025
Habari

Kumekucha Uzinduzi wa Washirika wa Tamasha, Tuzo Za Filamu Tanzania 2025

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Ngowi

DAR ES SALAAM: KAIMU Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Dkt. Gervas Kasiga amewataka wasanii kutunza vipaji vyao kwa kuwa ndio vinavyowapatia fursa ya vipato.

 Dkt.  Kasiga amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Washirika wa Tamasha na Tuzo za Filamu Tanzania 2025.

 Katika uzinduzi huo amesisitiza kuwa vipaji ndio sehemu kubwa ya kutoa ajira hapa nchini hivyo wasanii wavitunze.

Kwa maelezo yake tamasha hilo linaratibiwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bodi ya Filamu Tanzania pamoja na Studio 19 Limited.

Amesema tamasha hilo la nne toka kuanzishwa kwa matamasha kama hayo linapozinduliwa ubora wake utakuwa umeongezeka tofauti na matamasha mengine yaliyopita.

Amesema lengo la tamasha hilo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuanzisha na kuratibu program za kufufua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafila.

Amesema Rais Samia ameonesha ana mapenzi na tasnia ya filamu kwa kuwa hata yeye alishiriki katika kutengeneza filamu.

Akielezea mafanikio ya tamasha hilo amesema ni kutambua na kufufua vipaji mbalimbali vilivyojificha na kutolea mfano kama uandishi bora wa miswada, wapiga picha bora na mambo mengineyo.

Pia amesema tamasha limekuza hamasa kwa wadau wa filamu kuzalisha kazi bora zinazokidhi vigezo ndani na nje ya nchi.

Pamoja na kuwa na mchango katika kukuza ushirikiano na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Filamu 19, Sama Jahanpour amesema nguvu iliyokuwak wenye sanaa ya filamu ni nyenzo muhimu katika kueneza sanaa za masimulizi.

Pia amesema picha jongefu ina nguvu ya kufikia watu wengi, vile vile ina nguvu kubwa ya kuhamasisha watu.

 Mkurugenzi mwingine  wa Studio 19 Limited, Brian Paul amesema uzinduzi huo utawaweka wadau kutoka sekta mbalimbali za ubunifu pamoja ili kuorodhesha mustakabali wa tasnia hiyo.

“Tamasha la Filamu na Tuzo za Tanzania 2025 ni mpango kabambe unaolenga kuiweka Tanzania kama kitovu cha ubunifu wa kimataifa, kwa kutumia uwezo wa filamu kukuza utamaduni, kusukuma ukuaji wa tasnia na uvumbuzi wa nishati.

‘Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika safari hii, iliyoundwa ili kukuza mazungumzo, kuhamasisha ushirikiano, na kuoanisha malengo ya pamoja ya tamasha,” amesema..

Amefafanua kuwa tamasha hilo dhamira yake ni kutumia uwezo wa kusimulia hadithi kwa ajili ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Amesema tamasha hilo litafichua vipaji ambavyo havijatumiwa katika tasnia ya ubunifu, kuunganisha Washika dau mbalimbali na kukuza uwezo wa sekta hiyo kuleta mabadiliko yenye matokeo.

You Might Also Like

Nchimbi Agongelea Nyundo Kwa Wagombea Watoa Rushwa

Kichina Chatamba UDSM: Walimu Watanzania, Wachina Wapewa Tuzo kwa Umahiri

Miaka Minne Ya Samia, TANESCO Yajivunia Kudhibiti Upotevu Wa Umeme

Ujenzi Kiwanda cha Chumvi Waanza Lindi

Ajali ya treni Kigoma , abiria 70 wajeruhiwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Hatuwezi Kukwepa Matumizi Ya Bioteknolojia – Dkt.Nguvila
Next Article Kipanga: Lugha ya Kichina Inakuza Diplomasia, Kuimarisha Uhusiano
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?