MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kipaji pekee hakitoshi katika kufanya kazi za kihabari – Kipangula
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kipaji pekee hakitoshi katika kufanya kazi za kihabari – Kipangula
Habari

Kipaji pekee hakitoshi katika kufanya kazi za kihabari – Kipangula

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM: Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), imeweka bayana msimamo wa kisheria wa Sheria ya Huduma za Habari kuwa kipaji pekee hakitoshi kumfanya mtu afanye kazi za kihabari kama hajapitia katika taaluma ya Uandishi wa Habari na kukidhi vigezo.
Msimamo huo umebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula leo Jumatatu Machi 17 , 2025 jijini Dar es Saalam, wakati akizungumza katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One na kujibu swali la mmoja wa wasikilizaji aliyetaka kujua mamlaka ya Bodi katika kushughulikia walio kinyume cha sheria.
Wakili Kipangula amesema kama Serikali na nchi kwa ujumla imekubali kwamba Uandishi wa Habari ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine ni lazima kufuata matakwa ya kisheria.
Amesema kuwa hata kama mtu ana kipaji kikubwa kiasi gani, kama hajasoma taaluma ya uandishi wa habari haruhusiwi kisheria kufanya kazi za kihabari.
 “Kifungu cha 19 (1) cha Sheria ya Huduma za Habari, kinasema ‘Mtu hataruhusiwa kufanya kazi ya Uandishi wa Habari, isipokuwa mtu huyo awe amethibitishwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria’.
“Sisi Bodi, tunawashauri na kuwasisitiza wale wote wanaofanya kazi za kihabari bila kuwa na sifa waende shule, wakimaliza watarudi kuendelea na taaluma yao, uzuri ni kwamba mtu kama ana Shahada ya Udaktari anaruhusiwa kusoma Diploma tu ya Uandishi wa Habari, na huyu anaweza kuwa mwandishi mzuri wa habari za afya,” amesema.
Amesisitiza kuwa Serikali kupitia Waziri mwenye Dhama na Habari wakati huo, ilishatoa muda wa ziada wa miaka mitano ili wale  waliokuwa hawakuwa wamesoma warudi shule wakasome, na ulipoisha aliongeza tena mwaka mmoja.
Akijibu swali kuhusu wajibu wa chombo cha habari katika suala la mtangazaji au mwandishi kufanya kazi za kihabari bila kusomea taaluma, Wakili Kipangula amesema chombo cha Habari kina wajibu wa kuajiri watumishi/waandishi waliotimiza vigezo vya kitaaluma kwa mujibu wa Sheria.

You Might Also Like

PSSSF Yaanza Kulipa Mafao Kwa Kikokotoo  Kipya Kilichoboreshwa – Ridhiwani

PSSSF sasa kidijitali

Rais Samia azindua bwawa la umwagiliaji Mtibwa

Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa

Wakili Kanyama Achukua Fomu Mtumba

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Kulinda Wabunifu Wa Silaha
Next Article JAB Kusimamia  Mfuko wa Mafunzo kwa Waandishi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?