MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: JOWUTA Yataka Sheria Za Kazi Kuwalinda Wafanyakazi Katika Vyombo Vya Habari
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > JOWUTA Yataka Sheria Za Kazi Kuwalinda Wafanyakazi Katika Vyombo Vya Habari
Habari

JOWUTA Yataka Sheria Za Kazi Kuwalinda Wafanyakazi Katika Vyombo Vya Habari

Author
By Author
Share
3 Min Read

UTPC yaomba serikali kuingilia kati.

Mwandishi wetu

SINGIDA: CHAMA cha Wafanyakazi katika vyombo vya habari nchini(JOWUTA) kimetaka serikali kusimamia sheria za kazi kwa wafanyakazi katika vyombo vya habari kama zilivyo sekta nyingine ili waandishi wapate haki na stahiki zao.

Mwenyekiti wa Taifa wa JOWUTA,Mussa Juma ametoa wito huo wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC), mkoani Singida.

Juma amesema, waandishi wa habari wengi  nchini, wamekuwa wakipitia madhila makubwa ikiwepo kutoajiriwa ,kutokuwa na mikataba wala kuwa na bima za afya za Maisha.

“Sekta nyingine tunaona hatua zinachukuliwa kama mwajiri halipi mishahara wafanyakazi ama mwajiri anakaa na mtumishi zaidi ya mwaka bila kumpa hata mkataba,”amesema

Amesema JOWUTA imejitahidi mara kwa mara kufikisha hoja za maslahi bora ya waandishi serikali lakini bado hatua hazichukuliwi za kutosha.

“Kikubwa waandishi tusiwe wanyonge,tusione taaluma hii ni watu wenye shida ,tujitokeze kutetea maslahi yetu bila hofu kwanì taaluma hii haina tofauti na taaluma nyingine katika kupata kazi na haki za kisheria,”amesema

Juma amesema zaidi ya asilimia 80 ya waandishi nchini hawana mikataba ya ajira wala bima jambo ambalo linapunguza ari na uhuru  wa utendaji kazi wao.

Akizungumza katika mkutano huo,Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC,Kenneth Simbaya ameiomba serikali kulifanyia kazi suala la maslahi kwa waandishi wa habari.

Simbaya amemuomba aliyekuwa Mgeni rasmi katika mkutano.huo,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda kufikisha hoja za changamoto za waandishi katika baraza la mawaziri.

“Kama alivyosema awali Mwenyekiti wa JOWUTA sekta ya habari kuna changamoto nyingi tunaomba mnapokutana viongozi mlizumgumze na hili jambo la maslahi ya waandishi wetu, amesema

Hata hivyo, Juma amewasihi wanahabari nchini kuendelea kujiunga na JOWUTA ili kuwa na sauti ya pamoja kudai haki na stahiki zao.

Akizungumza katika mkutano huo,Profesa Mkenda ameahidi wizara yake kushirikiana na wanahabari nchini kwani anatambua umuhimu wa vyombo vya habari.

Amesema anazijua changamoto za wanahabari ikiwepo pia suala la kitaaluma na akaahidi kushirikiana na wadau kuboresha mitaala katika vyuo vya uandisbi wa habari.

Waziri Profesa Mkenda pia alizungumzia mabadiliko makubwa ya sekta ya elimu nchini ambayo yanalenga kuboresha sekta hiyo na kutoa wahitimu wenye ujuzi na uwezo kujiajiri na kuajiriwa.

You Might Also Like

Kanisa Lawashika Mkono Shule Ya Msingi Kibamba, Halmashauri Ya Ubungo

Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Kilele Kongamano la TEHAMA

Wagonjwa Wenye Maumivu Makali Kupatiwa Tiba Radiolojia MNH

Tanzania yajipanga kutumia nishati ya nyuklia kuzalisha umeme

Limeni mkonge unalipa – Maghali

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ridhiwani, Waziri Wa Kazi, Ajira UAE Waweka mkakati
Next Article Katibu Mkuu CCM Dkt. Nchimbi Akutana na Katibu Mkuu CRC
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?