Na Lucy Lyatuu
DAR ES SALAAM: JESHI la Polisi limemkamata na kumhoji kwa kina Amos Lutakulemberwa Lwiza (54) mkazi wa Tegeta Wazo Kinondoni kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu binti aliyefanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi, Muliro Jumanne amesema hay oleo Dar es Salaam na kuongeza kuwa taarifa hizo ni kuwa binti anayedaiwa kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji kwa kubakwa na kulawitiwa amekutwa amefariki suala ambalo sio kweli.
Amesema taarifa za binti huyo kufanyiwa vitendo hivyo zilitolewa mitandaoni hivi karibuni Agost 2024.
Kamanda Muliro amesema Jeshi hilo linatoa wito watu kujiepusha na kutoa au kuchapisha taarifa za uongo zenye malengo ya kuzusha taharuki katika jamii kwani kufanya hivyo ni makosa.
Amesema pia Jeshi hilo litaendelea kuzingatia maoni ya watu ambayo hayakinzani na sheria za nchi.