Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Author 19

Idara Ya Utafiti,Mipango Na Uwekezaji Tanesco Waaswa Kufanya Kazi Kwa Ubunifu

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeitaka Idara ya Utafiti, Mipango na Uwekezaji (PRI) kuongeza kasi katika utekelezaji wa mipango na miradi ya kimkakati, likisisitiza matumizi ya teknolojia, wataalamu wa ndani na uzingatiaji wa muda na mikataba ili kuongeza ufanisi wa katika utelelezaji wa miradi
Wito huo umetolewa na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita,  Jahulula Jahulula, akimuwakilisha Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Ziwa wakati akifunga Kikao Kazi cha Idara ya Utafiti, Mipango na Uwekezaji (PRI Forum), kilichofanyika kwa siku nne katika Ukumbi wa Rockcity Jijini Mwanza.
Habari Picha 13741
Habari Picha 13742
“Idara yenu ni injini ya TANESCO, kwa kuwa mipango ya miradi mikubwa ya uzalishaji na usafirishaji wa umeme, utafiti na uwekezaji inaanzia katika kazi zinazofanywa na idara yenu, hivyo mafanikio yake yana nafasi kubwa katika kuipeleka TANESCO na Taifa katika hatua za juu zaidi”. Amesema Mha.Jahulula
Aidha, Amepongeza watumishi wa idara PRI  kwa mchango wao katika utekelezaji na ukamilishaji wa miradi mbalimbali  ya kimkakati,ikiwemo Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere(JNHPP)lenye uwezo wa megawati 2,115, Mradi wa Umeme wa jua  wa Kishapu, njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma,  kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa njia ya ya kusafirisha umeme ya kilovoti 220 kutoka Mpomvu hadi mgodi wa GGM.
Habari Picha 13743
Habari Picha 13744
Amesema kupitia PRI, TANESCO pia inaendelea na miradi ya usafirishaji wa umeme wa kikanda, ikiwemo Tanzania-Zambia Interconnector (TAZA), huku maandalizi ya kuunganisha mifumo ya umeme ya Tanzania na Malawi, Msumbiji, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yakiendelea.
“Kila mmoja wetu sasa anapaswa kufahamu kuwa Shirika linamtegemea na nchi inamtegemea. Endeleeni kuchapa kazi kwa bidii, uzalendo na uadilifu,” animalize Mhandisi Jahulula.
Habari Picha 13745
Habari Picha 13746
Habari Picha 13747
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.