MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Gridi Ya Taifa Ni Dhaifu Kwa Mikoa Ya Kaskazini-Mramba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Gridi Ya Taifa Ni Dhaifu Kwa Mikoa Ya Kaskazini-Mramba
Habari

Gridi Ya Taifa Ni Dhaifu Kwa Mikoa Ya Kaskazini-Mramba

Author
By Author
Share
4 Min Read

Na Lucy Lyatuu

SERIKALI imesema gridi ya taifa ni dhaifu sana kwa mikoa ya Kaskazini ikisababisha kushuka kwa voltage na kwamba  mara nyingi inapozimika huanzia mikoa hiyo.

Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati, Felchesm Mramba amesema hayo Dar es Salaam akitoa ufafanuzi kuhusu Tanzania kununua umeme kutoka Nchini Ethiopia kwa ajili ya mikoa ya Kaskazini.

Amesema sekta ya Nishati wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi na ridhaa ya kuruhusu umeme kuingia kanda ya kaskazini kutokea nchi jirani.

“Ni uamuzi sahihi mno kwa sababu  wananchi wanaolia kwa kuwa na umeme mdogo watakuwa wamefanikiwa na pia upotevu wa umeme unaotokea kule Kaskazini utakuwa umeokolewa,” amesema.

Amesema hali ya umeme nchini sio kwamba hakuna changamoto lakini uzalishaji umeme wa kutosha nchini upon a kwamba hauchukuliwi kwa sababu kuna upungufu nchini.

Amesema sababu ya kuchukua umeme kwa ajili ya kaskazini ni kwamba hali ya umeme katika mikoa y akaskazini  ambayo  ni Kilimajnaro Arusha Manyara na Tanga ni kutokana na grid hiyo kuwa dhaifu.

“Umeme tunaozungumzia kwamba tunataka kuuchukua kwa Kaskazini ni kidogo sana sio mwingi ni Megawati 100 pekee na Mahitaji yote ya Kaskazini Megawati 700,” amesema

Amesema kwa sasa umeme unaozalishwa nchini  ni Megawati 3796 na umeme unaohitajika nchini Megawati 2200 na kusababisha kuwa na salio kubwa, kuna umeme mwingi wa ziada.

Mramba amesema mfumo w aumeme una vitu zaidi ya kimoja kwamba kiasi cha umeme n ahata ubora wa umeme,

Amesema kwa mikoa ya Kaskazini changamoto kubwa iliyopo kule ni kushuka kwa voltage  ambapo husababisha taa kuwaka kama kibatari.

Amesema tatizo ni kubwa sana huko na sababu  hiyo huanzia pale umeme unapoanzia hadi kwa mtumiaji iwapo umbali ni mrefu voltage hupugua  mpaka unapofika.

“Kwa Tanzania umeme wetu mwingi huzalishwa mikoa ya kusini,  kama Dar es  Salaam, Pwani Morogoro na kama mteja yuko Manyara inabidi kusafiri kwenda huko hivyo voltage hupungua njiani na zinaposhuka husababisha upotevu wa umeme,” amesema.

Amesema ili kutatua changamoto  hiyo ni kuweka chanzo cha kuzalisha umeme kwenye mikoa hiyo kuingiza umeme kwenye mikoa hiyo  kutokea kwenye mifumo mingine na Tanzania imepata umeme kutokea  nchini Ethiopia na kuingilia Namanga mkoani Arusha.

Amesema umeme utakapoingizwa pale ambao ni Megawati 100 utasababisha voltage inayokuw aimeshuka kupanda na kurudi kwenye kiwango chake na ule upotevu wa umeme unaopotea kule utaokolewa.

 

Amesema kwa kufanya hivyo wananchi wanaolia  voltage kushuka , mfumo mzima utarudi kawaida na kutumika ipasavyo.

Aidha amesema upotevu wa umeme unaopotea kule kaskazini, Megawati  17  zitakuwa salama. Ule umeme unaotakiwa kuingizwa sio jambo la ajabu na nchi na nchi kuuziana umeme sio jambo la ajabu.

Amefafanua kuwa Tanzania inanunia umeme nchi tatu ambazo ni Zambia ambao umeme wake unatumika mkoa wa Rukwa, Uganda na umeme wake hutumika  mkoa wa Kagera na Kenya ambapo umeme wake hutumika eneo la Horohoro wilaya ya Mkinga.

Kuhusu umbali wa kuingiza umeme kutoka Ethiopia amesema sio kwamba unachukuliwa kule moja kwa moja bali mita itaunganioshwa na  nchi ya Kenya ambapo utapita na kuunganishwa eneo la Namanga.

“Kati ya sisi na Ethiopia lazima kuishirikisha Kenya,  kwamba wao Ethiopia waanachia Megawati 100 inaingia kwenye Grid ya Kenya lakini sio za kwao, hivyo Ethiopia anafunga mita mpakani mwake kati ya Kenya na  Namanga pia itafungwa mita”, amesema.

Amesema chanzo cha umeme ni Ethiopia na malipo yatafanyika huko nan chi ya Kenya italipwa kiwango kidogo cha kutoa huduma ya kupitisha umeme.

Kuhusu kukamilika  kwa Bwawa la Nyerere amesema makubaliano hayo yako pande mbili, kuna wakati Tanzania itachukua na kuna wakati nchi itapeleka ila hali ya kaskazini kwa sasa  umeme utachukuliwa .

 

You Might Also Like

Tumeridhika na kazi za TTCL – Mwanaisha

Afrika ijadili changamoto sekta ya utalii – UN

Mafanikio Ya TEA Kwa Serikali Awamu Ya Sita;Miradi Ya Elimu 3,768 Yatekelezwa, Bil. 49.5 Zatumika

AU yataka vyombo vya habari Afrika, kulinda Uhuru wa vyombo vya habari 

Rais Samia Awasili Mwanza Kilele Cha Mbio za Mwenge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wananchi Wachukue Hatua Iwapo Hawajaridhika Na Huduma-TCF
Next Article Trilioni 1.2 Kumaliza Tatizo la Maji Dar
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

JAB Yatoa Mwezi Moja Kuthibitishwa, kupewa vitabulisho
Habari May 22, 2025
Hali Ya Ulinzi Na Usalama Wa Mipaka Ni Salama
Habari May 22, 2025
Ulega Ataka Ushirikiano Miradi Ya Kimkakati Ikamilike Kwa Wakati
Habari May 22, 2025
Aloe Dorotheae, Mmea Unaopatikana Tanzania Pekee
Habari May 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?