MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: FCC Yapongezwa Kukabili Bidhaa Bandia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > FCC Yapongezwa Kukabili Bidhaa Bandia
Habari

FCC Yapongezwa Kukabili Bidhaa Bandia

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
– Mwenyekiti Mlimuka Atembelea Banda la Sabasaba
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Tume ya Ushindani (FCC), Dkt. Aggrey Mlimuka, ameipongeza tume hiyo kwa juhudi madhubuti inazochukua katika kudhibiti bidhaa bandia na kukuza ushindani wa haki sokoni.
Amesema mafanikio hayo ni sehemu ya jitihada za serikali kulinda walaji na kuimarisha mazingira ya biashara nchini.
Dkt. Mlimuka alitoa pongezi hizo alipotembelea  Maonesho ya 49 ya Kibiashara yajulikanayo kama Sabasaba mkoani Dar es Salaam alipotembelea banda la Tume ya Ushindani (FCC).
Banda hilo liko ndani ya eneo la Wizara ya Viwanda na Biashara, mkabala na banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Akizungumza na wafanyakazi wa FCC waliopo kwenye banda hilo, Dkt. Mlimuka amesisitiza umuhimu wa tume hiyo kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya bidhaa bandia na umuhimu wa ushindani wa haki katika ukuaji wa uchumi.
“Tume imekuwa ikifanya kazi nzuri kwa kuhakikisha kwamba bidhaa bandia zinadhibitiwa na ushindani wa haki unalindwa. Hii ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda vyetu na ustawi wa mlaji wa kawaida,” amesema.
Amesema Maonesho ya Sabasaba ni jukwaa muhimu kwa taasisi kama FCC kuelimisha wananchi kuhusu majukumu yake na kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha soko huru na lenye uwiano wa ushindani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa FCC, Roberta Feruz, amesema ushiriki wa FCC katika maonesho hayo unaendelea kuleta mafanikio makubwa katika kuelimisha umma kuhusu haki zao kama walaji na wajibu wao katika kusaidia kudhibiti bidhaa haramu sokoni.
 “Tumekuwa tukipokea wananchi wengi wanaokuja kutaka kufahamu namna ya kutambua bidhaa bandia, haki zao wanaponunua bidhaa, na namna ya kutoa taarifa iwapo wana mashaka na bidhaa fulani. Hili linaonyesha mwamko mzuri,” amesema.

You Might Also Like

Katambi Ahimiza Udhibiti wa Bidhaa Duni, Jamii Yatakiwa Kutumia Huduma za TBS

Ridhiwani akutana na Mtendaji Mkuu ATE

Abiria Mil 2.51  Wasafirishwa Na SGR Kuanzia Julai 2025 Hadi Sasa

VETA Kihonda Waja Na Mashine Ya Kusaga Chumvi Sabasaba

VETA Yang’ara Sabasaba

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Manyara Kusambaza Mitungi 16,275 ya Gesi kwa Bei ya Ruzuku
Next Article Pato la Mwananchi Lapanda Tabora
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Kijaji: Huduma ya Kudungwa na Nyuki Kuongeza Kinga Yavutia Bungeni
Habari May 15, 2026
Serikali  Kutumia Fursa  ya AFCON,  Miss World Na IPU Kukuza Utalii Nchini
Habari May 15, 2026
TFS Yavunja Rekodi Utalii Wa Misitu,Mapato Yapaa Kwa Asilimia 43
Habari May 15, 2026
Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO
Habari May 14, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?