MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt. Ikomba Wa CWT Asema, Walimu Wanafanya Kazi Zaidi Bila Kulipwa Stahiki Zao
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt. Ikomba Wa CWT Asema, Walimu Wanafanya Kazi Zaidi Bila Kulipwa Stahiki Zao
Habari

Dkt. Ikomba Wa CWT Asema, Walimu Wanafanya Kazi Zaidi Bila Kulipwa Stahiki Zao

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Dkt. Suleiman Ikomba amesema walimu nchini wamekuwa wakiachwa pembeni bila kulipwa stahiki za masaa ya ziada ya kazi pamoja na posho ya ufundishaji, hali ambayo si sawa.
Dkt. Ikomba ametoa kauli hiyo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, katika kikao cha Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kilichofanyika jijini Dodoma.
Amesema suala la Posho ya ufundishaji limeainishwa wazi katika Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009, kifungu (L)2 kifungu kidogo cha 21, kinachotamka kuwa stahiki za malipo ya masaa ya ziada ya kazi ni halali kisheria kwa watumishi wa umma, wakiwemo walimu, ingawa kwa vitendo hazitekelezwi.
Habari Picha 11128
Ameeleza kuwa walimu wanahudumiwa na vyombo visivyopungua vitano vinavyohusika na uamuzi na utekelezaji, hali inayosababisha vyombo hivyo kukwamishana.
Amesema hali hiyo imekuwa kikwazo katika kufikiwa kwa maono na maslahi ya walimu na inahitaji kuangaliwa upya.
Pia Dkt. Ikomba amesema kitaaluma na kimaadili, mwalimu anatakiwa kuwahi kufika shuleni kabla ya wanafunzi.
Habari Picha 11129
Ameeleza kuwa walimu hufika shuleni saa 12 asubuhi ili kuwapokea wanafunzi na mara nyingi huondoka saa 10 au 10:30 jioni.
“Hata hivyo, licha ya kufanya kazi zaidi ya saa rasmi, walimu hawapati malipo ya saa za ziada wala  Posho ya ufundishaji, jambo ambalo haliko sawa,” amesema.
Aidha, amesema suala la
malimbikizo ya madai ya malipo na upandishwaji wa vyeo limeanza kupoteza mwelekeo.
Habari Picha 11130
Amebainisha kuwa awali kulikuwa na utaratibu mzuri wa kupandisha vyeo mwezi Julai, lakini kwa sasa walimu hupandishwa katika miezi tofauti kama Julai, Agosti au Septemba bila mpangilio unaoeleweka.
Ameshauri kuwa utaratibu huo wa awali uzingatiwe.
Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022, kifungu cha 13 kikisomwa pamoja na Kanuni za mwaka 2009 kifungu (L)2, Dkt. Ikomba amesema baadhi ya malipo ya likizo na posho ya kujikimu yamekuwa yakisahaulika na yanapaswa kulipwa kwa wakati.
Vilevile, amesisitiza kurejeshwa kwa vyombo halali vya kisheria kwa ajili ya majadiliano, ili walimu washirikishwe kikamilifu katika maamuzi yanayohusu utekelezaji wa masuala yao.
Habari Picha 11131
Amesema walimu ni kioo cha jamii na nguzo ya taifa kupitia elimu, hivyo anayestahili heshima apewe heshima.
Katika hatua nyingine, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua Waziri anayesimamia Wizara ya Vyama vya Wafanyakazi.
Habari Picha 11127
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amesema uimara wa CWT ni uimara wa sekta ya elimu Tanzania.
Amesema jumla ya walimu 415,719 wamepandishwa madaraja na walimu 110,038 wamelipwa madeni ya mishahara yenye thamani ya Sh. Bilioni 125.16, hatua inayothibitisha dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha maslahi ya walimu nchini.
Habari Picha 11133

You Might Also Like

Tanzania Na Namibia Kuongeza Juhudi Kukuza Ushirikiano Wa Kiuchumi

Mazao Ya Mikunde Yatajwa Kuwa Na Kiwango Kikubwa Cha Protini

Madiwani  Saidieni Wananchi Njia Sahihi Ya  Kutoa Taarifa Za Hitilafu Za Umeme-Mpogolo

Serikali Yaeleza Mikakati Ya Kuwezesha Vijana Katika Soko La Ajira

TARI Yawafikia Wakulima Kilosa, Kilimo Shadidi Cha Mpunga

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Pinda Aitaka Jamii Kujikita Upandaji Miti Bila Kusubiri Matukio Maalumu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Pinda Aitaka Jamii Kujikita Upandaji Miti Bila Kusubiri Matukio Maalumu
Habari February 6, 2026
Tanzania Yaongeza Kasi ya Utafutaji Masoko ya Parachichi Ulaya
Habari February 6, 2026
Umeme Vitongojini Wachoche Uchakataji Mazao Katavi
Habari February 6, 2026
Taska Mbogo Aitaka Serikali Kurejesha Viwanda, Kuimarisha Kilimo
Habari February 6, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?